Nafasi Ya Matangazo

March 11, 2018


Msanii wa Maigizo Yvone Sherry maarufu Monalisa Akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele Mkoani Mtwara Katika Moja ya Onesho la sanaa za Maigizo ya Jukwaani Kuhusiana na Changamoto zinazowakumba Wanafunzi wa Kike.

Wakufunzi wa Sanaa ya Maigizo ya Jukwaani Pinja Hanton na Niina Sillanpaa kutoka nchini Finlanda Finland Wakiongea na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya naliendele Kuhusiana na Sanaa Hiyo
Ari Koivo Mkurugenzi wa shirika la LiiKery-Sports& Development la Finland akiongea na wanafunzi wa Sekondari ya Naliendele kuhusiana na majukumu yanayofanywa na shirika lake.
Mwenyekiti wa Waigizaji Tanzania BONGO MOVIE Elia Mjatta akitoa mafunzo ya Jinsi ya Ushirikishwa katika sanaa ya maigizo ya Jukwaani.
************
Ili kupunguza Changamoto zinazomkabili Mwanafunzi hasa wa KikeShirika la Sports Development Aid SDA Limefundisha Sanaa ya Jukwaani walimu wa shule kumi za Mkoa wa Mtwara Manispaa na Mtwara Vijijini kwa lengo la Kuwafundisha wanafunzi Madhara ya Mimba za Utotoni.

Shirika Hilo ambalo Linawatumia wakufunzi waliobobea katika sanaa za Jukwaa kutoka Nchini Finland tayari limenza kuzunguka mashulni na kukagua kwa jinsi Gani Mafunzo waliyoyatoa yameweza kuwafikia wanafunzi kupitia walim wa Michezo waliokwisha kupewa Mafunzo.

Katika mafunzo hayo Walimu walipewa Fursa ya kuandaa mada ya Igizo Kuhusiana na Changamoto za Mimba mashuleni zinazowakabili na baadaye Kuonesha Igizo kwa njia ya Sanaa za majukwaani kwa lengo la Kutatuz Changamoto zinazotokana na Mila na Desturi za Jamii Husika.

Thea Swai ni Meneja Mradi wa SDA anasema Muda wa Kufanya Mafunzo kwa Njia ya Vitendo ni mdogo kwa wanafunzi kutokana na Baadhi ya shule Kushindwa kutenga Ratiba maalum kwa ajiili ya wanafunzi kuweza Kufanyia mazoezi na Kufikisha Ujumbe.
Posted by MROKI On Sunday, March 11, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo