Nafasi Ya Matangazo

March 06, 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso, Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon, wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon
 ******************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza uhuru wa mawasiliano kwa kuzindua huduma kabambe na ya kipekee kwa wateja wake wanaopiga simu na kutuma sms kwenda mtandao wowote nchini.

Taarifa iliyotolewa na Airtel leo kuhusu bando za ‘Yatosha Mitandao yote’  imesema Airtel imeamua kupunguza gharama kwa kuongeza thamani ya bando hizo kwa kumpa mteja MARA MBILI zaidi ya ilivyokuwa awali huku taarifa hiyo ikibainisha kuwa punguzo hilo kabambe limekuja kufuatia  serikali hivi karibuni kupunguza tozo kubwa za gharama za kuunganisha simu zinazokwenda mitandao mingine (Interconnection rate)

Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema “Airtel tumeona ni vyema  kuwapa wateja wetu fursa ya kufurahia punguzo hilo kupitia huduma hii itakayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Wateja wote watapiga na kutuma sms mtandao wowote nchini baada ya kujinunulia bando nafuu ya shilingi 1000 au bando mpya ya shilingi 600 tu.
https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif
Colaso amesema bando za ‘Yatosha Mitandao Yote’ bado zinaendelea kuwa bando bora kuliko zote nchini kwa kuwawezesha wateja wa Airtel kujipatia dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu saa 24, hapo awali kifurushi hiki cha shilingi 1000 mteja alipata dakika 25 tu. Huwezi kupata hii mtandao wowote, Vilevile tuna ifurushi kipya kilichoongezwa faida ili kumpa mteja dakika 16, 2MB na 50 sms  kwenda mitando yote kwa shilingi 600 tu. Zaidi ya hapo wataendelea kujipatia vifurushi nafuu vya SIKU, WIKI au MWEZI kwa kujiunga kwa kupiga *149*99# kisha chagua YATOSHA MITANDAO YOTE au kujiunga kupitia huduma ya Airtel Money na kufurahia Uhuru wa kuongea.

“Tunaipongeza serikali yetu kwa kupunguza gharama za kuunganisha simu mitandao mingine kutoka Shilingi 26.96 kwa dakika hadi shilingi 15.6 kwa dakika kuanzia januari, Airtel tunaona fahari sana kuwapa wateja wetu unafuu huo kupitia huduma yetu ya Yatosha Mitandao Yote. Mteja anatakiwa kuwa tu na laini iliyosajiliwa ya Airtel ili kufurahia huduma zetu bora na nafuu” aliezeza Colaso 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema  imeboresha  huduma ya bando za Yatosha ili kupanua uhuru  kwa wateja kutumia huduma Mitando Yote. Ukiwa na Airtel Yatosha mahitaji yako ya mawasiliano yametimia!

“ili kujiunga na Yatosha Mitando Yote, wateja watatakiwa kupinga *149*99# halafu changua 3 ili kununua bando ya ‘Yatosha Mitandao Yote’ kulingana na mahitaji yako. Tuna uhakika kuwa huduma ya Yatosha Mitandao Yote itarahisisha maisha” alisisitiza Bi Singano

Yatosha Mitandao Yote ni moja ya bidhaa za Airtel Yatosha, Airtel hivi karibuni pia ilizindua bando za intaneti za Yatosha SMATIKA Intaneti ambayo inatoa 2GB kwa Tzs 2000 ambazo zinadumu kwa siku 3. Wateja wa Airtel wanaojiunga na Smatika bando wanajishindia simu mpya za smartphone, modem na 1GB kwa wateja 1000 kila siku.
Posted by MROKI On Tuesday, March 06, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo