Nafasi Ya Matangazo

February 28, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hossea Ndagala akishirikiana na mafundi katika ujenzi wa msingi wa Zahanati ya Kijiji cha Ruhuru Wilayani humo.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
WANANCHI wa Kijiji Cha Ruhuru Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wamejitolea kuanza ujenzi wa Zahanati itakayo gharimu zaidi ya milioni 50 ilikuweza kutatua changamoto ya kutembea zaidi ya saa tatu kufuata huduma za Afya hali inayopelekea wengi wao kupoteza maisha kwakukosa huduma hiyo.

Wakizungumza jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Wawilaya hiyo Kanali Hosea Ndagala, kukagua ujenzi wa Zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za Wananchi, wananchi hao waliiomba serikali kuchangia jitihada hizo walizo anzisha za kujenga msingi na kuinua ukuta ilikuweza kumaliza tatizo hilo walilonalo la ukosefu wa kituo cha Afya na Zahanati.

Bahati Kimpaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ruhuru, alisema Kijiji hicho kina wakazi 2016 wameamua kuanzisha ujenzi wa Zahanati hiyo baada ya kuona Wananchi wanapata shida ya huduma ya Afya hasa wajawazito, ambapo usafiri mkubwa ni piki piki kwenda umbali wa masaa mawili na baadhi wanalazimika kutembea kwa miguu umbali wa masaa matatu kufuata huduma katika Vijiji vya Gwarama, Nyakayenzi na Nyanzige na endapo mwananchi atakosa fedha anashindwa kwenda na wengine kupoteza maisha.

Alisema hali hiyo iliwaumiza sana na kuamua kuweka mkutano Wa wananchi na kukubaliana kuanzisha ujenzi huo , baada ya kulifikisha halmashauri walifanyiwa tathimini na walipewa eneo ambapo fharama zilizo kadiliwa ni kiasi cha shilingi milioni 54 ambapo Wananchi walitakiwa kukusanya asilimia 20% kwa kukusanya tofari na mawe serikali iwajengee baada ya kuona wanauhitaji mkubwa wa zahanati hiyo wameamua kuanza kujenga wenyewe kabla ya serikali.

Kwa upande wake Nesia Semagogwa mkazi wa Kijiji hicho alisema kipindi cha nyuma wanawake walikuwa wakipimiwa ujauzito kwenye gari lakini kwa kipindi hiki gari hilo halikuwa linakuja kijijini hapo hali iliyowatia uchungu kutokana na wenzao wengi kupoteza maisha na kuamua kushirikiana na viongozi wao katika ujenzi wa Zahanati ilinawao waweze kupata huduma kama vijiji vingine.

" tunatoka hapa kwa miguu kwenda Kijiji cha tatu ambacho ni Nyakayenzi yani tunatumia muda mrefu na tunachoka sana tunaenda tunarudi jioni tunashinda na njaa yani suala hili linatuumiza sana tunatamani zahanati hii iishe mapema iliiweze kutusaidia na sisi tunateseka mno jamani mtusaidie kumaliza na sisi tuepukane na adha hiii", alisema Semagogwa.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alowapongeza wananchi hao kwa kujitoa katika ujenzi huo na kuahidi kuwapatia mifuko 20 ya simenti yeye binafsi na kwamba kuna fedha kiasi cha shilingi milioni 100 zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa vituo vya Afya zitatolewa kwaajili ya kijiji hiki muweze kumalizia Zahanati na kununua vifaa kutokana na changamoto waliyonayo.

"Moja ya changamoto mliyoiona ni changamoto ya Zahanati niwashukuru kwa hilo na sisis kama serikali tutawaunga mkono na Serikali inataka kila Kijiji kiwe na Zahanati na kata kuwa na Kituo cha Afya mmeonesha mfano katika Wilaya ya kakonko nyie ndio watu wa kwanza kujenga zahanati wenyewe na serikali ndio inacho kitaka hiki nyinyi mkijenga wenyewe mtasimamia ipasavyo na hamtamfumbia macho yeyote atakae jitokeza kufanya uharibifu kwakuwa mnauchungu nayo niwapongeze kwa hilo", alisema Kanali Ndagala.

Hata hivyo Kanali Ndagala amewaagiza Wananchi na viongozi wa vijiji vingine kuiga juhudi hizo serikali inahitaji wananchi kuwa na umiliki wa miradi lazima waanze kwa juhudi zao na kuahidi kuwapeleka Wananchi wanaosua sua kuchangia shughuli za maendeleo kwenda kuangalia wenzao walioanza kujitolea ilikuweza kupata zahanati yao binafsi ni jambo la kuigwa na wananchi wote.
Posted by MROKI On Wednesday, February 28, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo