Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2018

1
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa mwalimu Kahwa Mpunami wa Misungwi High ambao wameshinda (BEST FEMA CLUB OF THE YEAR 2017) Klabu Bora ya mwaka 2017 kutoka shule ya sekondari ya Myunzi Korogwe Tanga baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika kongamano la kujadili namna ya kupunguza ukatili wa Kijinsia kwa watoto wa kike likiwa na kauli mbiu ya "Ukatili wa Kijinsia sasa BASI" na kushirikisha Klabu mbalimbali za FEMA kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania , Kongamano limemalizika leo na lilikuwa likifanyika kwenye hoteli ya Seascape Mbezi Beach jijini Dar es salaam kwa siku nne mfurulizo, Kongamano hilo limehusisha pia mafunzo ya mambo mbalimbali. , Katika picha anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
2
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akikabidhi zawadi kwa Mayombo Lutego ambaye ameshinda (BEST FEMA CLUB MENTOR OF THE YEAR 2017) .kutoka shule ya Sekondari ya Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutangazwa mshindi katika kipengele hicho katika anayeshuhudia ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
3
Upendo Abisai kutokamwanachama wa Youth For Change Project uliopo chini ya Plan International Tanzania akitoa mada katika kongamano hilo kutoka kushoto ni watoa mada wengine Lydia Charles Mtangazaji wa Kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show, Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig, Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip na Koshuma Mtengeti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childrens Dignity Forum (CDF) BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.

4
Koshuma Mtengeti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childrens Dignity Forum (CDF) akitoa mada katika kongamano hilo kutoka kulia ni Lydia Charles Mtangazaji wa Kipindi cha FEMA TV SHOW, Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig na Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip.
5
Nicodemus Nangale kutoka shule ya sekondari Minaki kulia na Patrick Okilindi kutoka Shule ya Sekondari Arusha wakisoma habari iliyomhusu mmoja wa vijana kutoka Mkoa wa Mara aliyebadilisha maisha yake baada ya kumnyanayasa mke wake kwa kumpiga mara kwa mara.
6
Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Femina Hip akichangia mada katika kongamano hilo.
17
Halima Shariff Mjumbe wa Bodi ya Femina Hip akijadiliana jambo na Lydia Charles Mtangazaji wa kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show katika kongamano hilo kushoto ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania.
7
Lydia Charles Mtangazaji wa kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show na Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig wakijadili jambo katika kongamano hilo kutoka kushoto ni Dr. Minou Fuglesang Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Femina Hip Tanzania na Halima Shariff Mjumbe wa Bodi ya Femina Hip.
8
mmoja wa wanachama wa Klabu za Fema Hip akiuliza swali kwa watoa mada wakati kongamano hilo lilikendelea.
9
Amabilis Batamula Mkurugenzi wa Habari Fema Hip akifafanua jambo katika kongamano hilo.
10
Baadhi ya wanafunzi shule mbalimbali za sekondari nchini kutoka klabu za Fema Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
11
Lydia Charles Mtangazaji wa kipindi cha Fema TV Show na Fema Radio Show akihitimisha mjadala katika kongamano hilo kabla ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali.
12
Baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka klabu za Fema Hip zilizopo katika shule za sekondari hapa nchini wakiwa katika kongamano hilo.
13
Baadhi ya wafanyakazi wa Femina Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
14
Mkuu wa Maendeleo na Ushirika kutoka Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallstig akizungumza na vijana mbalimbali wananchama wa klabu za Fema Hip wakati wa kongamano hilo.
15
Baadhi ya wafanyakazi wa Femina Hip wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
16 18
Picha mbalimbali hapa chini zikionyesha baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi wanachama wa klabu za Femina Hip wakiwa katika picha za pamoja.
19 20 21


Kongamano la kumi la Fema Clubs kutoka kote nchini limemalizika leo jijini Dar es Salaam likiwa limekutanisha wanafunzi zaidi ya mia moja pamoja na walimu wao. Hawa ni wawakilishi kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Hili ni tukio ambalo shirika la Femina Hip hulifanya kila mwaka kama sehemu ya kuwaongezea uwezo vijana wanachama wa Clubs za Fema na pia walimu wao walezi, katika kutekeleza azma ya kuleta mabadiliko ya tabia na kujenga kizazi kinachozingatia mitindo bora ya maisha.

Kila mwaka kongamano huongozwa na mada maalum, na kwa mwaka huu kauli mbiu ni Ukatili wa Kijinsia Sasa Basi. Kauli mbiu hii inaakisi mkazo unaowekwa na shirika pamoja na wadau wake kupambana na matukio na tabia ambazo huwaumiza watu kwa sababu ya jinsi zao. Toleo jipya la jarida la Fema limesheheni simulizi za kweli na uzoefu wa watu ambao ama walifanya ukatili au walifanyiwa, lakini sasa wanasimama na kutuhimiza sote kuukataa ukatili wa kijinsia. Toleo hili lilizalishwa pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo UNICEF, CDF na Plan International, na kama anavyosema Mkurugenzi Mkuu wa Femina Hip, Dr Minou Fuglesang, “Juhudi zetu hizi ni sambamba na juhudi za serikali kutokomeza ukatili dhidi ya wananawake na watoto kama zilivyoainishwa katika mpango wa kitaifa uliozinduliwa mwaka jana.”

Mafunzo na mijadala ambayo ilifanyika wakati wa kongamano hili ililenga kuwaandaa wana Fema Club kuwa vinara wa mabadiliko, kuongoza mchakato muhimu wa kuelimisha jamii zao na kuhamasisha tabia zinazopingana na ukatili huu.

Femina Hip inaamini katika usawa, usawa wa kijinsia na kwamba hakuna mwenye haki ya kumbagua au kumuumiza mtu mwingine kwa sababu ya jinsi yake, rangi au kwa kuwa ana ulemavu.

“Tunaamini katika mabadiliko, mitazamo chanya na mabadiliko ya tabia. Ni jukumu la Femina Hip kuwawezesha vijana kupata taarifa zinazoweza kuwahamasisha kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao, wakahoji mila zenye madhara na wakajenga kizazi chenye usawa na ustawi wa sasa na baadae,” anasema Amabilis Batamula, mmoja wa wawezeshaji.

Baada ya siku tatu za mafunzo na mijadala, siku ya nne ya kongamano ni siku ya kusherehekea mafanikio na kuwapongeza wale ambao walifanya vizuri zaidi mwaka jana, 2017. Tunzo zilitolewa kwa Club bora kitaifa, mwalimu mlezi bora wa club kitaifa, mtandao bora wa Club za Fema, mlezi bora wa mtandao wa Club za Fema na Club bora kwa kila mkoa.

Washindi na vipengele vilivyowapa ushindi ni kama ifuatavyo BEST FEMA CLUB OF THE YEAR 2017 ilijishindia Klabu ya MISUNGWI HIGH FEMA CLUB, MWANZA Katika kipengele cha BEST FEMA CLUB MENTOR OF THE YEAR 2017 amejishindia Bw. MAYOMBO CHARLES LUTEGO wa MNYUZI SECONDARY SCHOOL, TANGA na katika kipengele cha BEST FEMA CLUBS NETWORK imejishindia klabu ya KILIMANJARO FEMA CLUBS NETWORK na mwisho ilikuwa ni kipengele cha BEST FEMA CLUBS NETWORK MENTOR ambapo amejishindia Bw.RENATUS SANGI wa MARA NETWORK

Posted by MROKI On Friday, February 02, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo