Nafasi Ya Matangazo

January 22, 2018

TANZIA: Familia ya Bwana Sylvester Manase Matunda Lema, wa Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000 jijini Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, Bibi.Lulu Sylvester kilichotokea katika Hospitali ya Agha Khan tarehe 20/01/ 2018 majira ya saa 10;30 alfajiri.

Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000. 

Mwili utaagwa Jumatano Januari 24, 2018 kuanzia saa 8 mchana Kanisani KKKT Usharika wa Sinza -Kumekucha. 

Mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Alhamisi tarehe 25/01/2018 kuelekea Kijiji cha Nronga-Machame, wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.
Posted by MROKI On Monday, January 22, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo