Nafasi Ya Matangazo

January 22, 2018

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akizungumza na waandishi wa habari
 Watumishi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya. 
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, ameipongeza Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuboresha huduma za Afya ya mama na mtoto mkoani Mbeya.

Uboreshaji huo umefanyika kupitia mradi wa TUMAINI LA MAMA ambao umewezesha wanawake wajawazito 269,638 kujifungulia katika vituo vya Afya.

Lengo la mradi huo ni kuboresha Afya ya mama na mtoto ambapo kabla ya mradi huu wajawazito wengi walikuwa wakijifungulia majumbani.

Aidha kupitia mradi huo idadi ya kaya zilizojiunga na Bima ya Afya zimeongezeka. 

Makala mewataka viongozi wa Mbeya kushughulikia changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika utekekezaji wa mradi huo ikiwemo usimamizi wa mapato na huduma katika vituo vya Afya.

Pia amewaagiza viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha DAWA zinapatikana muda wote katika zahanati, vituo vya Afya na Hospitali za wilaya.

Amesema azma ya mkoa wa Mbeya ni kuboresha Afya ya msingi na hivyo uhamasishaji wa ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya uendelee na serikali kwa kushirikiana na wadau wanatafuta Mabati 125,000 kwa ajili ya zahanati 40 na vituo vya Afya 5.
Posted by MROKI On Monday, January 22, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo