Nafasi Ya Matangazo

January 18, 2018

Mwandishi wetu
MARA nyingi katika jamii kumekuwepo na neno linalotumiwa la ‘presha’ likiwa na maana wasiwasi na kutojiamini. Na hii imekuwa ikitumika pale mtu anapokabiliwa na wakati mgumu kwa jambo fulani.

Sawia na matumizi hayo, kuna pia wanaoelezewa kuwa wanaugua presha na wanatumia dawa. Namna neno hilo linavyotumiaka yawezekana likawa linasababisha utata.

Hata hivyo, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Utafiti Tukuyu mkoani Mbeya inaeleza kwamba unapozungumzia kuhusu presha unaimanisha shinikizo la damu au wengine hufupisha kwa neno ‘BP’, ikiwa ni kifupi cha maneno ya kiingereza ya ‘Blood Presure.’

Maana ya Shinikizo 
NIMR inasema kuwa shinikizo au presha ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo ukidunda. 

Kwa kawaida mtu anapopimwa huainishwa kwa vipimo viwili; presha ya systole na diastole.

Systole ni kipimo cha juu mfano 140 mm Hg ambacho hupima nguvu ya msukumo wakati moyo unadunda kusukuma damu.

Shinikizo au presha ya diastole ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa wakati moyo umepumzika au kati ya mapigo ya moyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA

Kinachosababisha shinikizo la damu 
NIMR inaeleza kwenye taarifa yake kuwa kinachosababisha shinikizo la damu ni unene wa kupindukia (Vitambi), matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula, kutoshughulisha mwili kwa mazoezi au kazi zinazotoa jasho, uvutaji wa sigara na unywaji pombe wa kupindukia.

Mambo mengine yanayoweza kusababisha ni mazingira ya mfadhaiko, msongo wa mawazo ama sonona, ulaji wa vyakula vingi vya wanga, sukari na mafuta na wakati mwingine historia ya familia kusumbuliwa na tatizo hilo. Hii ina maana tatizo linaweza kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. 

Jinsi ya kujikinga 
Kuna mambo mengi ambayo mtu anaweza kufanya ili kuzuia kupata shinikizo la damu. Miongoni ni kuacha matumizi ya tumbaku, kuwa na uzito unaowiana na urefu, fanya mazoezi ili kuimarisha hali ya afya ya moyo angalau mara tatu kwa dakika 30 kila wiki.

Mambo mengine ni kupunguza matumizi ya chumvi nyingi kwenye vyakula, punguza unywaji wa pombe na pia punguza ulaji wa vyakula vyenye wanga mwingi na ikiwezekana nafaka zisizokobolewa.

Mtu anapaswa pia kupunguza ya vyakula vyene mafuta mengi kupunguza uwezekano wa mwili kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu ama kama ilivyozoeleka kwa jina la kolestero.

Kwa watu wazima umri zaidi ya miaka 18 inabidi kupima shinikizo la damu mara kwa mara na kula vyakula vyenye vitamin kwa wingi kama vile matunda na mboga za majani.

Dalili za Shinikizo la Damu 
Kuumwa kichwa, uchovu, matatizo ya macho, kichefuchefu, kutapika, Hali ya woga, Hali ya kuchaganyikiwa, kupauka kwa ngozi au kuongezeka wekundu wa ngozi.

Dalili nyingine ni kukosa usingizi, kuhisi kizunguzungu, kuwa na hamu ya chunvi, kitambi, hasira mara kwa mara, kuwa na hali yakufanya vitu haraka na kukosa uvumilivu, kiharusi na kutokwa jasho sana.

Kudhiniti shinikizo la damu
Kula vyakula vyenye afya, punguza vyakula vyenye chumvi, mafuta, kolestero na wanga. Dhibiti mifadhaiko, kupunguza mifadhaiko au kutafuta njia ya kudhibiti mifadhaiko.

Fanya mazoezi; dakika thelathini ikiwezekana dakika 30 kila siku, kuwa na uzito sahihi kulingana na urefu na pata ushauri wa daktari au kuhudhuria kliniki napobainika unaugua shinikizo la damu.

Kutodhibiti shinikizo la damu ni rahisi kupata kiharusi, tatizo la kuona vizuri, kuharibika kwa mishipa ya damu na ubongo, moyo kushindwa kufanya kazi na matatizo ya figo.

Makala haya yameandaliwa na Chama cha Waandishi Wanaokabili Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TJNCDF) kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania (TDA). Maoni na ushauri tuma TJNCDF, S.L.P. 13695, Dar es Salaam.








Posted by MROKI On Thursday, January 18, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo