Mwandishi Wetu, TJNCDF
Shirikisho la Vyama vya
Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA) linaeleza kuwa karibu kila mtu
anakabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo.
Kinachosababisha hali hiyo,
TANCDA inaeleza kuwa ni hali ya jumla ya maisha. Mazingira na mifumo ya maisha
ambayo jamii inaishi yanachagiza binadamu kujikuta anapata msongo wa mawazo.
Kuna mambo mengi yanayoweza
kumsababishia mtu kuwa na msongo, na hapa TANCDA inayaelezea kwa mfumo wa
maswali.
Katika maswali hayo ukiona
miongoni yanakuhusu, unapaswa kuchukua tahadhari ili tatizo la msongo wa mawazo
lisikusababishie madhara.
Siyo rahisi mtu kujua madhara
anayopata kama yanatokana na msongo wa mawazo yanayomkabili kwa sababu hiyo
TANCDA inashauri jamii kuchukua tahadhari.
Miongoni mwa maswali mtu
anayoweza kujiuliza ni: Je, hatuwi na wasiwasi kuwa watu wanachunguza ngua tunazovaa?
Je, hatushikwi na hofu pale
tunapovuka barabara kuwa tunaweza kugongwa na magari? Je, hatuwi na wasiwasi
pale tunaposhindwa kumaliza kazi zetu kwa wakati? BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA.
Hayo ni baadhi tu ya maswali
ambayo mtu anaweza kujiuliza. Jambo ambalo mtu anapaswa kulizingatia ni kuwa
jambo lolote linalomsababisha mtu kuwa na hofu, woga, taharuki, kukosa raha au
kushindwa kutekeleza majukumu mengine ni sehemu ya mambo yanayomsababishia
msongo wa mawazo.
Je, tunapojikuta katika hali
hii tufanye nini? TANCDA inashauri njia rahisi za kukabiliana na msongo wa
mawazo ni kufanya mazoezi mara kwa mara na kuwa makini na jambo moja kwa wakati
mmoja.
Njia nyingine, TANCDA inaeleza
ni kumueleza mtu wako wa karibu na unayemuamini kuhusu tatizo lako ili
akusaidie kwa ushauri.
Hali nyingine ya kukabiliana na
msongo wa mawazo ni kucheka na kushiriki kwenye michezo, sherehe na burudani
kama vile harusi, ubatizo na mikusanyiko ya dini.
Mtu anapaswa kujifunza kukubali
kuwa hawezi kushindwa kila kitu na kutojitwika mambo mengi kuliko anavyoweza
kufanya kwa wakati.
Kuwa na muda wa utulivu kwa
dakika kadhaa na TANCDA inakushauri ni vyema ukachukua muda dakika chache kila
siku kwa kuzima simu hasa pale inapokufanya uwe na majukumu mengi.
Makala haya yameandaliwa na
Chama cha Waandishi Wanaopambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TJNCDF).
Maoni, ushauri au maswali tuma tjncdf@gmail.com au S.L.P 13695, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment