Nafasi Ya Matangazo

January 29, 2018

MUDA mfupi baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kutaja watu waliovamia maeneo ya hifadhi nchini hasa mkoani Arusha, familia ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa imejitokeza hadharani na kuzungumzia sakata hilo la baba yao kutajwa kuwa mimosa wawatu waliovamia maeneo ya hifadhi. 

Fredrick Lowassa ndie msemaji wa familia ambaae amezungumzia sakata hilo kwa masikitiko makubwa juu ya jina la Lowassa kutajwa Latika uvamizi huo.

"Nimesikia taarifa za Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha. 

Nimesikitishwa sana na matamshi hayo kutoka kwa waziri ambaye kwa mtu mwenye wadhifa wake kutoa kauli zisizo na msingi wowote na kulaghai Umma. 

Nimemfahamu Mhe Kigwangalla kwa miaka mingi, tangu wakati anavurugana na mbunge mwenzake wa Nzega na rafiki yangu Mhe Hussein Bashe kule Nzega.

Kwa maoni na mawazo yangu nimekuwa nikiamini kwamba Kigwangalla atakuwa mtu aliyebadilika na kujifunza kutoka na makosa yake ya nyuma.

Kauli yake ya leo ni ushahidi kwamba bado ana matatizo yale yale ya kukurupuka.

Ni wazi hata baada ya mambo mengi kubadilika na pengine nyakati za kuchafua watu kukoma, ndugu huyu bado anaishi nyakati zile zile.

Ni wazi Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais Magufuli , kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina Wataalamu na uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

Nikiwa kama Msemaji wa Familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa.

Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Waziri Kigwangalla hayapo, na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.
Posted by MROKI On Monday, January 29, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo