Nafasi Ya Matangazo

November 17, 2017

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
WATOTO wawili wa familia Moja wamefariki Dunia katika ajari ya Nyumba ya Majani maarufu kwa jina la  Ngondano iliyotokea katika Kijiji cha Luhuru Wilayani Kakonko  Mkoani Kigoma.

Akithibitisha tukio hilo Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho,Bahati Kimpaye alisema mnamo Novemba 12 mwaka huu  majira ya saa tano Asubuhi alipokea taarifa kutoka kwa Wananchi yaka kutokea  kwa ajari ya Nyumba ya Mkazi Mmoja kuungua na kusababisha kifo cha watoto wawili ambao ni Elizabeth Masumbuko (4) na Subira Masumbuko (2) waliokuwa wameachwa ndani ya Nyumba hiyo peke yao na Mama yao akiwa ameenda kuchota maji.

Kimpaye alisema alipofika eneo la tukio alikuta mabaki ya neti na miili ya watoto hao ikiwa imeungua vibaya sana , na kubaini chanzo cha ajari hiyo ni Moto ulioshika katika Nyumba ya Nyasi waliyokuwemo watoto hao na watoto hao baada ya Kuona moto waliingia ndani ya neti kujificha na kupelekea kicho chao.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala aliwaagiza Wananchi wote kujenga Nyumba bora za kuishi na kuacha tabia ya kuishi kwenye nyumba zilizo jengewa na majani zinazo hatarisha usalama wao na zilizopelekea kifo cha watoto ambao hawana Hatia .

Alisema inasikitisha sana na ni jambo la aibu Watu wananguvu za kuchukua udongo na kujenga nyumba nzuri za kuishi lakini Wengi wa Wanakijiji hicho Wanaishi katika Nyumba za majani hali inayo hatalisha maisha yao nakuwapotezea Watoto maisha na kushindwa kutimiza ndoto zao.

" nitoe agizo kuanzia leo sitaki kuona Nyumba za majani katika Wilaya hii kuliko kuishi kwenye nyumba hizi ni bora mkakaa nje ijulikane tu hamna Nyumba, kulikoko nyumba hizi inaumiza sana Kupoteza Watoto wetu kutokana na uzembe wa baadhi ya Watu nguvu za kujenga mnazo kama mmeshindwa basi muweke utaratibu wa kujengeana kwa awamu ili kijiji chote kiwe na nyumba zenhe ubora", alisema Kanali Ndagala.

Aidha Mkuu huyo aliwaomba Wananchi kuacha kuwakaribisha Wahamiaji haramu ambao Wengi wao hujenga Nyumba Za majani iliwatakapo fukuzwa wasipate hasara na Wengi wao wanasababisha Matatizo makubwa katika Vijiji wanavyo fikia , na watoe taarifa dhidi ya Wakimbizi wote.
Posted by MROKI On Friday, November 17, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo