Nafasi Ya Matangazo

November 23, 2017

Meneja wa Bandari Msaidizi, Bwana Elihuruma Lema (wa kwanza kulia) akimuonyesha Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Burundi Bwana Audace Niyonzima (wa pili kulia) viroba vya mbolea wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Burundi, Bwana Audace Niyonzima ameipongeza Mamlaka ya Usimamaizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja katika Bandari ya Dar es Salaam.

Niyonzima ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bandari hiyo, naipongeza TPA kwa kuboresha huduma zake katika bandari ya Dar es Salaam kwani sasa mteja anatumia muda mfupi kuchukua mzigo wake tofauti na zamani ambapo mteja alikuwa anapata mzigo wake baada ya siku nyingi, alisema Niyonzima.

Kamishina Mkuu huyo alitanabaisha kwamba, Burundi itaendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya mizigo yake kutokana na maboresho ya huduma na uhusiano wa kidugu ulipo kati ya Tanzania na Burundi. Pia alifurahishwa kuona shehena kubwa ya kahawa kutoka Burundi ikiwa inaandaliwa bandarini kwa ajili ya kusafirishwa kwenda ngambo.

Aidha Niyonzima alitoa wito kwa mawakala wa forodha kutoa huduma kwa uaminifu kwa wateja wao ili kutoharibu taswira nzuri ya bandari ya Dar es Salaam ambapo kwa sasa kila mrundi anavutiwa kutumia bandari hii. Ameahidi kwamba Burundi itaendelea kuimarisha uhusiano na kushirikiana na bandari ya Dar es Salaam kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari Msaidizi Bwana Elihuruma Lema, alimfahamisha Kamishina Mkuu huyo kwamba, TPA imedhamiria kwa dhati kuboresha huduma katika bandari ya Dar es Salaam. 

Kwa sasa TPA inatekeleza mradi mkubwa wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project ambao utahusisha ujenzi wa gati maalum la magari, uboreshaji wa gati namba 1  7, uongezaji kina, upanuzi na uimarishaji mlango wa kuingilia na kutokea meli (entrance channel) ili kujenga uwezo wa kuhudumia meli kubwa zaidi.

Posted by MROKI On Thursday, November 23, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo