Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2017



Katibu wa Afya, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, Stella Mwakikunga,  ambaye pia ni Mkufunzi katika Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanayotolewa chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nakuwahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, akitoa mafunzo hayo leo yakiwa katika siku ya nne mjini Dodoma.Picha:Mroki Mroki-DAILY NEWS Digital.
 
TANZANIA imetajwa kuwa nchi iliyofanikiwa kuwa na mfumo wa Kielektroniki uliojengwa na wataalamu wake wa ndani wenye uwezo wa kuunganisha vituo vya kutolea huduma kama Zahanati ,Shule, Vituo vya Afya na Hospitali zote nchini hali itakayowezesha kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Mtaalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Mradi wa Uimarishaji wa  mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Desderi Wengaa kuwa Tanzania imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa na wataalamu wenye uwezo wa kujenga mifumo ya kielektroniki itakayosaidia kuchochea maendeleo.

“Tanzania imekuwa nchi ya mfano Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika  na Afrika kwa kuwa na mfumo unaowezesha wananchi kutoa mrejesho wa  huduma wanazopata katika maeneo ya kutolea huduma hali itakayoongeza uwazi na uwajibikaji,” alisema Wengaa.

Mafunzo kwa watumiaji wa mfumo wa PlanRep yanawahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora.

Mikoa minginine nchi nzima tayari imeshapatiwa mafunzo hayo ambapo uzinduzi rasmi wa matumizi yake unataraji kufanyika mapema mwezi huu.

Mradi wa PS3 unatekelezwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na umejikita katika maeneo ya Utawala Bora na Ushirikishwaji wananchi, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha, Mifumo ya TEHAMA  pamoja na  Tafiti Tendaji, Tathimini na ufuatiliaji.


 Washiriki wa Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanawahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, wakiendelea na mafunzo hayoleo katika siku ya nne mjini Dodoma. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.

Ofisa kutoka Tamisemi, Ayoub Kambi ambaye pia ni Mkufunzi katika Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanayotolewa chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) na kuwahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, akitoa mafunzo hayo leo yakiwa katika siku ya nne mjini Dodoma.
 Mkufunzi Christopher Masaka akifundisha namna ya uendeshaji wa Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanayotolewa chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) na kuwahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, akitoa mafunzo hayo leo yakiwa katika siku ya nne mjini Dodoma.
Washiriki wa Mafunzo ya siku nane ya Uendeshaji Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) yanawahusisha Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Wachumi, Maafisa Mipango, Wahasibu, na Makatibu wa Afya, kutoka mikoa ya Manyara, Tanga, Dodoma, Singida na Tabora, wakiendelea na mafunzo hayoleo katika siku ya nne mjini Dodoma.
Posted by MROKI On Thursday, August 31, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo