Nafasi Ya Matangazo

July 17, 2017

SHIRUIKA  la Ndege la Kitanzania Precision Air Services Plc, leo limetangaza kuanza safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Kahama Mkoani Shinyanga.

Taarifa hiyo ilitolewa hapo jana wakati shirika hilo lilipo kuwa likifanya safari ya majaribio katika uwanja wa Kahama (KBH) kwa kutumia ndege yake yenye usajili namba 5H-PWF aina ya ATR42-500. 

Ndege hiyo ilitua katika kiwanja kidogo cha Kahama majira ya saa 11 jioni, ikiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu ikitokea Mkoani Mwanza. 

Akizungumza na wageni waalikwa pamoja na waandisi wa habari wakati wa tukio hilo, Meneja Uratibu na Mahusiano, Hillary Mremi alisema kwa kuanzisha safari za Kahama Precision Air inaendelea kutekeleza Kauli mbiu yake ya ‘Wewe ni Sababu Sisi Tunaruka’ kwa kufungua safari ambazo zimelenga kutatua mahitaji ya Wananchi. 

Mremi alisema Precisiona Air itaanza safari zake kuanzia tarehe 5 Septemba 2017, ikianza na safari tatu kwa wiki, Kila siku ya Juamatano, Ijumaa na Jumapili na kuongeza safari hizo hadi kila siku, kwa kuzingatia mahitaji ya soko.

“ Hakutakua na sababu ya ya abiria kutokea Shinyanga na Kahama kusafiri kwa magari hadi Mwanza kwenda kupanda ndege kwa safari za Dar es Salaam. Safari zetu kutokea Kahama sio tu zitaokoa muda bali hata gharama za usafiri kwa Wananchi wa kawaida na Wafanyabiashara. 

Uwepo wa safari hizi kunaongeza urahisi wa kufikika kwa maeneo mbali mbali ya nchi yetu na kukua kwa Dar es Salaam kama lango kuu na uchumi wetu kwa ujumla. Nimatumaini ya kuwa safari hizi zitafungua milango ya fursa kwa Kahama.”  Mrremi aliongeza.

Wakati huo huo Mremi aliishukuru Serekali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kahama, Fadhili Nkurlu kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Precision Air .  

‘Kwa niaba ya Uongozi wa Precision Air na Wanahisa, napenda kutambua ushirikiano tunaoendelea kuupata kutoka Serekalini,kupitia Mkuu wetu wa Wilaya,  Fadhili Nkurlu, ambaye bila kuchoka alihakikisha Uwanja huu wa ndege unakua tayari kwa safari hizi tunayo furaha kuwataarifu wananchi wa Kahama ujio wetu. 

Precision Air inatoa shukrani za dhati kwa Fadhili Nkurlu kwa juhudi zake zakuahakikisha uwanja huu unakua tayari kwa ajili ya kutoa huduma. Tunaunga mkono maono ya Raisi wetu, Dr. John Joseph Pombe Magufuli kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda na tunaamini kupitia huduma zetu tutaisaidia Nchi yetu kufikia malengo hayo. Alikaririwa Bw.Mremi 

Kahama inapatikana Kaskazin Magharibi mwa Tanzania inafahamika kwa machimbo ya dhahabu na inaaminika kua na Uchumi unakua kwa kasi, ilikosa huduma za usafiri wa ndege za uhakika. Kuanzishwa kwa safari za ndege za Precision Air kunatarajiwa kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi wWilayani Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla. 

Precision Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi,Shirika la ndege la Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika ya ndege ya nayoheshimika Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani na nje kuelekea sehemu takribani 11. 

Iktokea Dar es Salaam (makao makuu) Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar,Nairobi na Entebbe.
Posted by MROKI On Monday, July 17, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo