Nafasi Ya Matangazo

July 02, 2017

MIONGONI mwa Makampuni ambayo yamejitokeza mwaka huu kushiriki katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ni pamoja na Kampuni ya Mobisol kutoka nchini Ujerumani ambayo tayari imeanza kufanya shughuli zake hapa nchini Tanzania.

Kampuni hii inauza na kusambaza vifaa mbalimbali vya Umeme Jua (Solor Power) ambao vimekuwa suluhisho la kuachana na mwanga wa vibatari katika maeneo mengi ambayo hayana umeme nchini au yale ambayo hukatikakatika umeme mara kwa mara na kuwafanya wananchi kukosa mwanga na hata kutazama na kusikiliza taarifa muhimu za habari kupitia Televisheni na Redio. Lakini pia hata kuchaji simu zao. 

Father Kidevu Blog ilitembelea maonesho hayo ya Sabasaba yanayofanyika kwa mara ya 41 sasa na kuingia katika Banda la Karume na kukutana na Banda la Ujerumani ambalo limekaa na kampuni mbalimbali za Kijerumani. Miongoni mwao ni hawa Mobisol Tanzania.
 Umati mkubwa wa watu waliokuwa wakipatiwa maelezo mbalimbali katika banda hilo ndio kitu ambacho kilimvutia mwandishi wa Blog hii na kuingia katika Banda hilo kuweza kujua nini hasa kinafanywa na Mobisol Tanzania.

Huduma za bashasha zikamsogeza karibu na banda hilo na kukaribishwa na Mkurugenzi wa Mauzo wa Mobisol Tanzania, Robert Sanyagi na kutoa maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma zao.

Licha ya kuuza Panel na zao lakini pia Bobisol kwa kuzingatia hali ya ugumu wa maisha kwa Watanzania wanatoa huduma hiyo kwa njia ya Mkopo na kukupa vifaa vyao mbalimbali ambavyo vinapatikana kwa ugubwa tofauti na mteja kuweza kulipa kila mwezi hadi kwa miaka mitatu.
 Mraditi wa Mauzo wa Mobisol Tanzania, John Msaki (kulia) akihudumia wateja waliofika katika banda la Kampuni hiyo ya Solar Powoer.
 Hizi ni moja ya Televisheni wanazouza Mobisol Tanzania
 Wananchi wakipatiwa huduma
 TV hizo za Mobisol ambazo zinatumia nishaji ya Jua zinauwezo wa kuwaka hata kama haijaunganishwa na Panel yake kwa zimetengenezwa kwa mfumo maalum wa kuhifadhi moto kwa muda mrefu zaidi.
 Wateja mbalimbali walimiminika na kupatiwa huduma katika banda hilo.
 Mkurugenzi wa Mauzo wa Mobisol Tanzania, Robert Sanyagi (kulia) akihudumia wateja kwa kuwapa maelezo juu ya huduma zao.
 Betri za kuhifadhia moto za Mobisol
 Mobisol 'Sola Bora Maisha Bora' hizi ni aina nyingine za Televisheni zinazotumia nishati ya Jua walizonazo.
Usijaribu kulipita Banda hili bila kuingia a kupata habari za huduma zake.
Posted by MROKI On Sunday, July 02, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo