Nafasi Ya Matangazo

June 19, 2017


Watuhumiwa  James Rugemalila (kulia) na Harbinder Sethiwakiwa chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi na Magereza kabla ya kupandishwa kizimbani katika Mahakam ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
 Watuhumiwa  James Rugemalila (kushoto) na Harbinder Sethi wakiwa chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi  walipofikishwa kizimbani katika Mahakam ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
******************
WAFANYABIASHARA maarufu nchini, James Rugemalila na Harbinder Sethi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani milioni 22.1  na  Sh bilioni 309. Anaandika Fransisca Emmanuel wa Habarileo.

Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kusomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kadushi anayesaidiana na Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimbi na Joseph Kiula wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

Mashitaka yao ni kula njama, kujihusisha na mtandao na uhalifu, (kughushi na kutoa fomu zilizoghushiwa (yanamkabili Seth) kujipatia fedha kwa udanganyifu na kusababisha serikali hasara.

Rugemalila na Seth wamekosa dhamana hivyo wanaenda mahabusu hadi kesi yao itakapotajwa tena kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, haina mamlaka ya kusikiliza mashitaka ya uhujumu uchumi hivyo maombi ya dhamana yanatakiwa kupelekwa Mahakama Kuu.
 SOURCE: DAILY NEWS-HABARILEO BLOG
Posted by MROKI On Monday, June 19, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo