Nafasi Ya Matangazo

June 06, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
Baadhi ya wadau wa mazingira waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akizungumza jambo kwa wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira.
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste ProLtd, Abdallah Mbena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Mwenye shati nyeupe ni  Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark.
Baadhi ya wadau wa mazungira wakifanya zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.

Baadhi ya uchafu ukiwa kwenye mifuko yake mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Green WastePro Ltd  mara baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.
Posted by MROKI On Tuesday, June 06, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo