Nafasi Ya Matangazo

May 10, 2017

Baadhi ya walimu wa shule za Msing na Sekondari Manispaa ya Temeke.
BAADA ya miaka miwili ya majaribio, Twaweza kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na shirika la Innovations for Poverty Action (IPA), imedhihirika kuwa kuwalipa walimu fedha baada ya matokeo ya kujifunza kunaweza kuboresha matokeo ya kujifunza.

Matokeo ya utafiti unaojulikana kama KiuFunza, utafiti mkubwa wa aina yake Afrika Mashariki, yamewasilishwa Dodoma tarehe 10 Mei 2017 wakati wa tukio la kuwazawadia baadhi ya walimu bahshishi zao.Wabunge na viongozi kutoka wizara za Elimu na TAMISEMI walihudhuria akiwemo Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri waNchi – Ofisi ya Rais: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Kwa kipindi cha miaka miwili, Twaweza na IPA wamefanya majaribio yafuatayo katika shule 200 kwenye wilaya 21 za Tanzania:
  • Kutoa bahshishi kwa kujifunza stadi mahususi zilizoainishwa kwa darasakwenye kundi moja la shule (Stadi).
  • Kutoa bahshishi kwa ongezeko la kujifunza kwenyekundi jingine la shule (Mashindano).

Matokeo ya awali yanaonesha matokeo chanya ya kujifunza kwa wanafunzi. Njia zote mbili zilijaribiwa ili kulinganisha matokeo yaliyopatikana na kundi la shule zilizohusishwa moja kwa moja. Japokuwa mfumo waMashindano ni mgumu zaidi kueleweka kuliko Stadi, mfumo huu huleta usawa zaidi kwa walimu, kwakuwa wanafunzi hushindana na wenzaowalio kwenye makundi yenye uwezo unaofanana.. Stadi  hueleweka kwa urahisi zaidi lakini pia huwapa nafuu walimu wenye wanafunzi wenye uwezo mkubwa (mara nyingi wa shule za mijini).

Matokeo mengine muhimu ni:
  • Twaweza inawazawadia walimu 788wa masomo wa madarasa ya I, II, na III na walimu wakuu 135 kwa matokeo ya mitihaniya mwaka 2016.
  • Malipo hayo ya bahshishi ni shilingi 251,827,040.00. Asilimia 17 ya bahshishiililipwa kwa walimu wakuu na asilimia 83 yaani shilingi 209,855,867.00 zililipwa kwa walimu wa masomo.
  • Wastani wa bahshishi waliyolipwa walimu wa masomo ni Shilingi 266,315.00 sawa na karibu asilimia 42 ya wastani wa mshahara wa kila mwezi (kabla ya kodi) mwaka 2016.
  • Walimu tisa kati ya kumi kwenye shule za majaribio wanaunga mkono wazo la malipo kwa matokeo.

Mwaka 2016
  • Kulikuwa na shule 135 kutoka wilaya 21 zilizoshiriki kwenye utafiti na shule 60 zilitumika kwa ajili ya kulinganisha.
  • Jumla ya wanafunzi 65,643 walipimwa wakiwemo wanafunzi wa shule za ulinganisho.
  • Kwa ujumla, wanafunzi 48,042 walikuwa katika shule ambako motisha ilitolewa na hivyo walifanikiwa kujifunza zaidi kuliko wenzao.

Matokeo haya ni kutoka awamu ya pili ya KiuFunza 2015 -2016. Awamu ya kwanza 2013 – 2014 Twaweza ilifanya jaribio la kupeleka fedha za ruzuku moja kwa moja shuleni (ambapo kwa sasautaratibu huu unatumiwa na Serikali kuanzia Januari mwaka 2016) na Malipo kwa walimu ya matokeo ya kujifunza pekee na kwa kuchanganyarizuku na bahshishi. Awamu hii ya I ilionesha matokeo chanya ya kujifunza pale ambapo motisha kwa walimu na upelekaji wa fedha za ruzuku moja kwa moja shulenivilipochanganywa. Awamu ya pili ilijaribu mifumo makini zaidi ya utoaji wa motisha baada ya upelekaji wa Ruzuku ya uendeshaji wa shule moja kwa moja shuleni kuanza kutekelezwa na serikali.

Twaweza imechagua kujikita kwenye utoaji wa motisha kwa walimu katika awamu ya kwanza na ya pili ya KiuFunza kwasababu ushahidi kutoka maeneo mbalimbali duniani unaonesha kuwa motisha huwahamasisha walimu kuongeza jitihada nakuleta matokeo chanya ya kujifunza. Kwa kuongezea, KiuFunza (na tafiti nyingine) zinaonesha wazi kuwa motisha kwa mwalimu na uwajibikaji ni mambo yamekosekana shuleni. Wakati wa ziara za kushtukiza mwaka 2016:
  • 54% ya walimu walikuwa darasani wakifundisha.
  • 27% hawakuwepo shuleni.
  • 19% walikuwepo shuleni lakini hawakuwepo darasani kufundisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze, anasema, “Twaweza, kwa kushirikiana na IPA tumeonesha kuwa utoaji wa motisha kwa mwalimu unaweza kuboresha matokeo ya kujifunza. Japokuwa kujifunza kunachangiwa na mambo mengi, tumeonesha, kupitia utafiti wa kisanyansi, kuwa kuchanganya motisha na uwajibikaji kunaweza kuleta matokeo mazuri ya kujifunza kwa watoto. Tuna ushahidi thabiti wa kile kinachoweza kufanyikana kuwa na uhakika kuwa tukifanya hicho watoto watajifunza. Changamoto kubwa ni namna ya kuwafikia watoto wengi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kufanya mpango huu kudumu kwa muda mrefu. Kutokana na serikali ya awamu ya tano kujikita katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wa kawaida, tuna imani kuwa utafiti huu utapokelewana matokeo yake kukubalika katika ngaziza juu za Serikali.”
Posted by MROKI On Wednesday, May 10, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo