Nafasi Ya Matangazo

April 21, 2017

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wamiliki wa majengo kulipa kodi za majengo kabla ya Juni mwaka huu ili kukwepa kulipa faini kutokana na kuchelewa kulipa kodi hiyo.


Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo wakati, akifungua mkutano mkuu wa. Klabu ya Waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC).


Kayombo amesema kuwa ni vyema wamilikinwa,majengo wakalipa kodi hizo,kwa hiyari badala ya kusubiri kupigwa faini jambo ambalo hata mamlaka hiyo haitaki kifikie huko.


"Tayari viwango vya kodi hizi vimeshatolewa kwa maeneo yaliyopimwa lakini piabyale ambayo hayajapimwa, tunakusanya kodi ili kuiwezesha serikali katika kutoa huduma mbalimbali," amesema kayombo.


Naye, Jane Mihanji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandushi wa dar es Salaam, amesema , mkutano wao unalenga kujadili masuala mbalimbali na namna ya kuboresha tasnia ya habari nchini.


Amesema ushirika wa TRA katika mkutano huo ni katika kuhakikisha wanahabari wanapata uelewa zaidi kuhusu masuala ya kodi ili waweze kuelimisha jamii kuhusu ulipaji wa kodi kwa hiari ili kulerta maendeleo.


Aidha, aliwataka waandishi kutumia kalamu zao ipasavyo ili kuijenga Tanzania kiuchumi kwakuwa waandishi wakiandika vizuri juu ya masuala ya kulipa kodi, itasaidia kupatikana kwa huduma zote muhimu.
 Mwenyekiti wa DCPC, Jane Mihanji akizungumza.
 Maofisa kutoka TRA
 Wajumbe wa DCPC wakifuatilia mkutano
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwakawa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) ulioanza  jana, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa DCPC, Jane Mihanji na Kulia ni Makamu wake, Shedrack Sagati.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwakawa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) ulioanza  jana, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa DCPC, Jane Mihanji
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwakawa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) ulioanza  jana, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa DCPC, Jane Mihanji na Kulia ni Makamu wake, Shedrack Sagati. (Picha na Mroki Mroki).
 Makamu Mwenyekiti wa DCPC , Shedrack Sagati akizungumza na wajumbe juu ya kul;ipa ada zao kwa wakati.
 Makamu Mwenyekiti wa DCPC , Shedrack Sagati akizungumza na wajumbe juu ya kul;ipa ada zao kwa wakati.
Posted by MROKI On Friday, April 21, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo