Nafasi Ya Matangazo

April 24, 2017



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (wapili kulia) akizindua rasmi tawi la DCB benki mjini Dodoma hii leo. Tawi hilo la kwanza la Benki hiyo nje ya jiji la Dar es Salaam na la 10 lipo katika jengo la Mfuko wa LAPF. Kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu, John Samwel Malecela, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Benki, Prof Lucian Msambichaka(wapili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Benki, Edmund Mkwawa
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela akifungua akauinti katika Benki hiyo mjini Dodoma leo huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akimwangalia (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Benki, Edmund Mkwawa akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi hilo jipya na la kwanza la Benji hiyo mjini Dodoma ambapo  alisema kwa sasa benki ina mawakala wapatao 231 waliosambaa Dar es Salaam na kwaupande wa Dodoma wamefanikiwa  kupata mawakala 38 ambao muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma karibu zaidi na wananchi.
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mzee Mashuhuri Mjini Dodioma akizungumza wakati wa kutoa neno la ukaribisho na baraka kwa ujio wa Benki ya DCB.
 **********
 Na Mroki Mroki-TSN Digital
BENKI ya DCB imezindua tawi lake la kumi na la kwanza nje ya jiji la Dar es Salaam hii leo katika Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma.

Akizindua tawi hilo mjini Dodoma leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene alipongeza uongozi wa DCB Banki kwa uamuzi wao wa kufungua twi hilo mjini Dodoma ikiwa ni harakati moja wapo za kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Dodoma.

Aidha alisema kufunguliwa kwa tawi hili la Dodoma zitasogezwa huduma za kibenki karibu na wafanyabishara na wakaazi wa mji wa Dodoma.

“Haya ndiyo maendeleo tunayotaka katika sekta ya kibenki ili huduma za benki zipatikane kwa urahisi zaidi kwa wananchi na nina hakika wananchi wengi watapata huduma bora kupitia tawi hili,” aalisema Waziri Simbachawene.

Waziri Simbachawene aliwaasa wafanyabiashara, Wafanyakazi na wakazi wote wa mkoani Dodoma watumie fursa hiyo kwa kufungua akaunti mbalimbali za DCB kupitia tawi hilo jipya na la kwanza la Benki hiyo nje ya jiji la Dar es Salaam kwa kile alichoamini kuwa huduma zitakozotolewa na tawi hili zitakuwa bora na zenye kumjali mteja.

Pia Waziri huyo wa TAMISEMI aliwaasa viongozi wa Manispaa ya Dodoma kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili mfuko wa Wanawake na Vijana na kuingia mkataba na DCB ili waweze kuratibu utoaji wa mikopo hiyo kwa niaba yao kwa riba nafuu ya asilimia 10.

“Kwakua sasa DCB Benki ipo mjini Dodoma na imeonyesha mafanikio makubwa sana ya uendeshaji na usimamizi wa mikopo hii mkoani Dar es Salaam, nina hakika itasaidia sana kuwahudumia wajasiriamali wengi mkoani Dodoma,”alisema Waziri Simbachawene.

Mapema akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Banki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka alisema tawi hilo litatoa huduma za kibenki kwa wakazi, Wafanyabiashara na wafanyakazi wa Dodoma na maeneo jirani.

“Tunatoa wito kwa wakazi wote wa Dodoma na vitongoji jirani, mtupokee na muwe mstari wa mbele kutumia huduma za benki tawini hapa ili kukuza tawi hili na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia wananchi wengi zaidi katika suala zima la kupiga vita umasikini,”alisema Prof Msambichaka.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Benki, Edmund Mkwawa, alisema katika kipindi cha miaka 15 ya utoaji huduma bora,  benki hiyo imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuwa karibu zaidi na wateja wake, kubuni huduma mbalimbali kulingana na matakwa ya wateja kama vile, huduma za kibenki kupitia mawakala (DCB Jirani) na  kupitia simu ya mkononi (DCB Pesa).

Mkwawa alisema kwa sasa benki ina mawakala wapatao 231 waliosambaa Dar es Salaam na kwaupande wa Dodoma wamefanikiwa  kupata mawakala 38 ambao muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma karibu zaidi na wananchi.

Mbali na Dodoma, DCB Benki inampango wa kupeleka huduma za DCB mikoa mingine kupitia DCB Jirani kama vile mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kahama, Mtwara, Arusha, Iringa na Mbeya huku lengo likiwa kuwa na mawakala 1,500 nchi nzima kufikia mwezi Disemba mwaka huu.
Posted by MROKI On Monday, April 24, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo