Nafasi Ya Matangazo

March 05, 2017


Meneja wa Dawasco Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka
***********
 Na Mwandishi wetu
WAMILIKI na watumiaji wa maji ya visima hususani wakazi wa Ilala jijini Dar es salaam wametakiwa kujitokeza ili kuunganishiwa huduma ya Majisafi yanayotolewa na shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO).

Wito huo wa Dawasco umelenga kuwasaidia wananchi wa maeneo mbalimbali kuondokana na hujuma inayofanywa na wamiliki wachache wa visima binafsi vya Maji dhidi yao na shirika.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa kuunganishia wamiliki wa visima katika mfumo rasmi wa Dawasco.

Akielezea juu ya mpango huo, Kaoneka alisema kwa kipindi kirefu  kiasi cha maji kilichokuwa kinazalishwa hakikuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wote hususani wakazi wa Ilala, hivyo kupelekea watu wengi kuchimba visima vya maji binafsi.

“Tulikuwa na changamoto ya utoshelezaji wa Maji kwa maeneo mengi ya mji. Uzalishaji Maji haukuwa mkubwa hivyo kwa wananchi wengi iliwalazimu kuchimba visima vyao binafsi ili wapate huduma hiyo,”alisema Kaoneka.

Aliyataja maeneo ambayo yanaongoza kuwa na visima vingi kuwa ni vinavyotoa huduma ya maji safi ni  na vinamilikiwa na watu binafsi kuwa ni Kariakoo, Upanga na katikati ya Mji.

“Kwa sasa uzalishaji wa maji umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka kiasi cha lita za ujazo milioni 182 hadi lita za ujazo milioni 270 kwa siku, hivyo kupelekea maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kuwa na utoshelezi mwingi wa maji.
“Nitoe rai kwa wamiliki wote wa visima katikati ya mji kuja ofisi za Dawasco ili kujiunga rasmi na mtandao wa majisafi. Aidha tumegugundua wengi wa wamiliki wa visima hufanya maunganisho ya maji bila kufuata taratibu husika na mwisho hudai yale maji ni ya kisima wakati Dawasco tukishayapima tunagundua ni ya Dawasco,” aliongeza Kaoneka.

Aliwataka wananchi kutoa kutoa taarifa za watu wanaohujumu miundombinu ya dawasco kwa kutoa taarifa ktika ofisi zao mbalimbali.

Posted by MROKI On Sunday, March 05, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo