Nafasi Ya Matangazo

March 17, 2017

Na Bety Alex, Arusha
Chama cha mawakili Tanganyika TLS kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa urais wa chama hicho kesho ambapo hadi sasa wagombea watano wamejitokeza kugombea  nafasi hiyo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea  jijini Arusha rais mstaafu  anayemaliza  muda wake John Seka amesema uchaguzi wa mwaka  huu umekua na hamasa kwakuwa umehusisha wagombea ambao wanafahamika zaidi na jamii na pia umefanyika kwenye sheria mpya za
uchaguzi wa chama.

Seka amewataja wagombea hao maarufu kuwa ni Tundu Lisu,Fransis Stola,Laurence Masha,Victoroia Mandarin na Godwin Mwapongo.

Aidha Seka amewataka wanasheria kuzingatia misingi ikiwa ni pamoja na kuisaidia na kuishauri  serikali katika utungaji wa sheria za bunge na mahakama   na ili kuongeza nguvu katika kuwasaidia wanyonge na wasio na  uwezo waweze kupata haki.

Amewataka wanachama wa chama hicho kujitathimini ni kiongozi gani atakayefaa kupigiwa kura ili aweze kukabidhiwa kijiti cha kuongoza chama hicho.

Kwa upande wake wakili wa kujitegemea dr  Eva Hawa Sanare amewataka wanasheria kusoma sheria mpya ya katiba ya  Kenya low society kwa kuwa wanasheria  bado hawajaelewa utawala wa sharia Wajiendeleze ili  kuepuka kesi ambazo hazijakamilika kwani baadhi yao wamekuwa wakiendesh akesi  ambazo hazijakamilika Amesema kuwa bila wanasheria kufanya kazi yao na kuielewa kwa undani hawataweza kuendeleza majukumu yao ya kuisaidia jamii
Posted by MROKI On Friday, March 17, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo