Nafasi Ya Matangazo

March 20, 2017

Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo (kushoto) akiwa katika uzinduzi wa mradinwa usambazaji umeme vijijini (REA) awamu ya tatu mkoani Mbeya leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo hii leo katika kijiji cha Ilinga, Wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Pamoja nae ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
VIJIJI 238 vya mkoa wa Mbeya vitanufaika na umeme wa REA awamu ya tatu imebainishwa.

Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameyasema hayo hii leo katika Kijiji cha Ilinga, Wilayani Mbeya wakati akizindua awamubya tatu ya mradi huo wa kupeleka umeme vijijini.

Waziri Muhongo amesema serikali imekusudia kupeleka Umeme katika Vijiji 12,000 katika awamu hii nchi nzima, na kuwawezesha wananchi kupata nishati hiyo.

Akizungumza na wananchi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla asema endapo Vijiji 238 vitapatiwa umeme kupitia mradi huo vitafanya idadi ya vijiji vitakavyokosa umeme kuwa nane pekee.

"Endapo awamu hii mtavipatia vijiji 238 umeme basi katika mkoa wangu ni vijiji nane tu vitasalia, hivyo nawaomba na vyenyewe mviingize kwenye mradi ili ifikapo 2020 Mkoa wa Mbeya usiwe na Kijiji kisichokuwa na Umeme,"alisema Makalla.

Amesema Mkoa wa Mbeya ni wazalishaji wakubwa wa chakula na uongezaji thamani hivyo wa mazao ya kilimo hivyo  umeme ni nishati muhimu ambayo inahitajika mkoani humo.

Aidha  amenuomba Waziri  Prof Muhongo na Shirika la Umeme nchini Tanesco kushughulikia tatizo la kukatika mara kwa mara kwa umeme mkoani humo na kuathiri shughuli za uzalishashaji viwandani,   Uwekezaji na hata kwa wananchi wa kawaida.

Katika kutatua kero hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo amemuagiza Meneja wa Tanesco Kanda na Mkoa kushughulikia tatizo la kukatika Umeme mara kwa mara.
Posted by MROKI On Monday, March 20, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo