Nafasi Ya Matangazo

March 05, 2017

Na Bety Alex Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amefanya ziara ya kukagua miradi ya maji,zahanati na barabara kwenye kata ya Kisongo tarafa ya mukulati halmashauri ya wilaya ya Arusha mkoani Arusha iliyo lenga kutatua kero na changamoto zinazo wakabili wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Engorora alisema kuwa serilika ya awamu ya tano imewekeza kwa wananchi kwa asilimia kubwa ndio maana tunaona viongozi wanatoka maofisi kwenda kusikiliza matatizo ya wanachi ili kutekeleza wajibu wao kulingana na sera ya hapa kazi tuu ili kuweza kulikomboa taifa kuepukana na wimbi la umaskini.

Gambo alisema kuwa mabosi walio waweka madarakani ni wananchi hivyo viongozi wanapaswa kushindana kupambana na kero za wananchi na wataakikisha wanatatua na kutekeleza wajibu wao ili  kuletea maendeleo ya kweli kwa wananchi ili kutekeleza   dhamira ya serikali ya Rais magufuli iliyo lenga kuwajali wananchi wanyonge na wakipato cha chini ambapo alisema serikali  aitawafumbia macho viongozi wavivi,wazembe na wasio wajibika kutekeleza wajibu wao .

Gambo amewataka wananchi kufanyaka kazi kwa bidii hili kuepukana na wimbi la umsikini ambapo itasaidia kujenga uchumi imara kwa wananchi kupata  uduma muhimu kwa haraka  ilikuweza kujitegemea na kujenga uchumi imara ambao taifa litaweza kufanya shughuli zao bila kutegemea misaada ya nchi zingine duniani ambazo ziumekuwa zikisaidia kwenye sekta mbalimbali za kielimu,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

Wakizungumza na Waandishi hapo juzi wananchi wa kijiji cha Engorora walisema kuwa uhaba wa ukosefu wa maji kwa muda mrefu umesababisha wananchi kwenda kutafuta maji kutoka bomba la jeshi la wananchi monduli [Jwtz] ambayo yamekuwa yakitoka mara mbili kwa wiki jambo ambalo alitoshelezi maitaji ya maji kwa wakaazi wa eneo hilo.

Walisema kuna mradi wa maji unaofadhiliwa na benki ya dunia ambao umelenga kutoa uduma kwa kijiji cha Loovilukuny ulioanza tangu mwaka 2o14 lakini bado haujakamilika na gharama za mradi huo ni shilingi million 87,000,000/ ambao unasimamiwa na ofisi ya wilaya kama wakikamilisha kwa wakati itapunguza kero ya maji kwa vijiji vya kata ya kisongo.

Sambamba na hilo wananachi wa kata ya kisongo wamaendelea kupaza sauti kwa mkuu wa mkoa kwenye suala la upatikanaji wa umeme vijijini [REA] bado ujafikia vitongoji vingi kwa kipingi kilicho pita. “Tunaomba msukumo wako mkuu wa mkoa ili kufikia utekelezaji wa awamu ya Tatu ‘ umeme usambazwe katika vitongoji na kaya zote ususani katika maeneo ya huduma za jamii kama shule, vituo vya Afya na zahanati “.

Aidha wamemuomba mkuu wa mkoa kuongea na mamlaka ya ujenzi wa barabara,nyumba na majengo [ TANROAD] ili kuweka matuta maeneo hatarishi katika barabara  kuu kwani ni hatari kwa wananchi wavukao kwa miguu eneo la waya.
  Arusha

Posted by MROKI On Sunday, March 05, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo