Nafasi Ya Matangazo

March 04, 2017

Mtandao wa Jinsia (Tanzania Gender Network Programme- TGNP) umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga nakwa ajili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 2 na Machi 3 mwaka 2017 katika ukumbi wa Vijana Center katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga pia yamewakutanisha waandishi hao wa habari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa vilivyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni mwezeshaji Bi Nyanjura Kalindo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya kijinsia na kuwakutanisha na wanaharakati wa masuala ya kijinsia kutoka kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ili kuongeza nguvu ya pamoja.
“Vipaumbele vya TGNP ni vitano ambavyo ni afya,elimu,kilimo,uziduzi na maji hivyo kwa kuwapatia mafunzo waandishi wa habari tunaamini kabisa itaongeza chachu kuandika habari kwa usahihi zaidi kuhusu masuala ya kijinsia”,alieleza Kalindo.
Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Rasel Madaha aliwaomba waandishi wa habari kufika katika maeneo ya pembezoni kwani vitendo vya ukatili wa kijinsia yapo na hayaandikwi hali inayosababisha vitendo hivyo kuendelea kujitokeza na kuwafanya baadhi ya watu kuendelea kunyanyasika.

 Picha ya pamoja baada ya mafunzo 
 Picha ya pamojaPicha ya pamoja ,wawezashaji wa mafunzo hayo,Rasel Madaha (kushoto) na Nyanjura Kalindo na Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC)

Picha na Frank Mshana,Stephen Wang'anyi na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Posted by MROKI On Saturday, March 04, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo