Nafasi Ya Matangazo

March 14, 2017

 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala akipita katika shamba la bangi katika kitongoji cha Nyangereke ambapo baade shamba hilo walilifyeka na kuchoma moto.
Na Cosmas Makalla
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Col.Hosea Ndagala ameteketeza shamba la bangi zaidi ya heka moja na kukamata watuhumiwa wawili wanaosadikiwa Kulima zao la bangi katika kijiji cha Mbizi kitongoji cha Nyangereke wilayani Kakonko siku ya Jumatatu.

Watuhumiwa waliokamatwa katika shamba  hilo la bangi ni bwana David Maganye (55) mkazi wa mbizi ambaye alikutwa shambani hapo na kueleza kuwa yeye ni Mlinzi wa shamba hilo. Aidha mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa ni bwana Kasindi Hamisi mkazi wa Mbizi ambaye alidai shamba hilo ni lake.

Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia oparesheni ya Mkuu wa Wilaya pamoja na vyombo vya dola ikilenga kutokomeza zao la bangi ambalo ni Madawa ya kulevya yenye madhara makubwa kwa jamii.

‘Wananchi wanatakiwa kulima mazao ya chakula siyo bangi', alieleza Col.Ndagala baada ya kuteketeza shamba hilo la bangi na kuwasisitiza viongozi wa Vijiji kuhakikisha hakuna mwananchi anayelima bangi.

Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa wananchi wanalalamika kuwa wana njaa lakini wanalima bangi hivyo  Serikali ina mkono mrefu na macho mengi itawafuata wanaolima bangi popote. Aliwasisitiza wananchi kutunza misitu na kuacha kukata miti katika mlima kwa madhumuni ya kilimo kwani uoto wa asili unaharibika.

Oparesheni ya kutokomeza Madawa ya kulevya hususani bangi inaendelea chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya na vyombo vya usalama katika maeneo yote ya Wilaya ya Kakonko hivyo wananchi wanasisitizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi ilimkuepuka kuchukuliwa hata za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani na endapo wakikutwa na hatia watahukumiwa kwenda jela.

Watuhumiwa waliokamatwa wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa ajili ya upelelezi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani hivi karibuni.
Posted by MROKI On Tuesday, March 14, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo