Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2017


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi,Richard M. Kayombo
 
UHAKIKI WA TIN DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru  wananchi na wafanyabiashara  wote wa Mkoa wa Dar es Salaam  kwa ushirikiano walioutoa wakati wa zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo awamu ya kwanza ya zoezi hili ilianza rasmi tarehe 16/08/2016 na kuhitimishwa tarehe 31/01/2017. 

Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali imebainika kwamba baadhi ya wananchi walishindwa kukamilisha zoezi hilo katika muda uliopangwa.

Mamlaka inapenda kuwatangazia wakazi wote wa Dar es Salaam kuwa wale wote wenye TIN ambazo hazikuhakikiwa wanapaswa kutembelea ofisi za Mamlaka katika Mikoa yao ya Kodi kwa maelekezo ya uhakiki. 

Tunapenda kusistiza kwamba wahusika watalazimika kuhakiki taarifa zao kabla ya kupata huduma zifuatazo:
1.    Kulipia ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazotoka na kuingia Nchini
2.    Kuhuisha leseni za udereva
3.    Kulipia ada ya mwaka ya  gari
4.    Kulipa kodi nyinginezo zinazosimamiwa na Mamlaka
5.    Kupata cheti cha uhalali wa ulipaji kodi (Tax Clearance Certificate)

Kwa wananchi walioko nje ya nchi kwa sababu mbalimbali katika kipindi cha uhakiki, wanafahamishwa kwamba watahakiki pindi watakaporudi nchini kwa kuonesha vielelezo vya kuthibitisha wa kutokuwepo nchini.

Baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya uhakiki kwa mkoa wa Dar es Salaam, Mamlaka itaendelea na awamu ya pili katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani. Zoezi litaanza rasmi tarehe 15/02/2017 na kumalizika tarehe 31/03/2017. Tarehe ya kuanza kuhakiki katika mikoa mingine iliyobaki itatangazwa baadae.

Pia kwa watakao bainika kuwa na TIN zaidi ya moja, utaratibu uliopo ni wa kuhuisha taarifa ya mojawapo ya TIN hizo na kuzifunga nyinginezo.  Endapo mtu ana madeni ya kodi katika mojawapo ya TIN hizo au zaidi, utaratibu wa kudai madeni utaendelea kwa mujibu wa sheria na Mamlaka haitamzuia mwenye deni kuhakiki TIN yake. 

Mamlaka inatoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kukamilisha zoezi hili kwa wakati. Pia tunawakumbusha wananchi wote kuwa lengo la zoezi hili ni kuhuisha na kupata taarifa sahihi za mlipakodi na si vinginevyo.

Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali usisite kuwasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800750075/0800780078 au Barua pepe huduma@tra.go.tz
 ‘’Pamoja Tunajenga Taifa Letu’’
 Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
Posted by MROKI On Thursday, February 02, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo