Nafasi Ya Matangazo

February 24, 2017

Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza hii leo na kukasema watanzania wasiwe na hofu juu ya afya yake.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, wakati Mzee Mwinyi alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam jana.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, wakati Mzee Mwinyi alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam jana.


Na Mroki Mroki
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezengumza na TSN Digital na kuwatoa hofu watanzania juu ya afya yake na kusema kuwa yupo vizuri na wala hasumbuliwi na maradhi yoyote.

Rais Mstaafu Mwinyi alizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati alipomtembelea na kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya, nyumbani kwake Upanga hii leo.

“Ah Mimi niko vizuri nina afya njema na leo nimefanya mazoezi yangu kama kawaida kwa kutembea kilometa tano kwa mwendo wa kasi, hivyo niwatoe hofu watanzania na wananchi kwa ujumla juu ya afya yangu,”alisema Alhaji Mwinyi.

Jana katika mitandao ya kijamii kulienezwa tarifa kutoka nchini Marekani ambako walisema Rais huyo alikuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo na kufariki Dunia jambo ambalo si la kweli na kiongozi huyo yupo mwenye afya njema.

Aidha tarifa kutoka idara ya Habari Maeleozo kupitia Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas ilikanisha tarifa hizo na kusema kuwa Mzee Mwinyi ni mzima wa afya, anaendelea na majukumu yake kama kawaida.

“Jana alihudhuria chakula cha jioni kuadhimisha siku ya Taifa la Kuwait na leo mchana baada ya swala ya Ijumaa alimtembelea kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya,”ilisema tarifa hiyo.

Dk Abbasi aliitaka jamii ifahamu kuwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015, kwa mtu yeyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari za uongo au uzushi katika mitandao.
Posted by MROKI On Friday, February 24, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo