Nafasi Ya Matangazo

January 24, 2017


Na FK Blog Kigoma,
SHIRIKA la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)  kupitia shirika linalosimamia Shughuli za mazingira kambi za Nduta na Mtendeli na Vijiji vinavyo zunguka kambi (REDESO) limekabidhi Pikipiki nne, Kompyuta moja  pamoja na mafunzo kwa Madiwani vyenye thamani ya shilingi milioni 16.8 kwa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko lengo ikiwa ni Kuwawezesha maafisa Wa Maliasili kupita katika maeneo ya misitu iliyo haribiwa na Kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa Wanawake na Vijana.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Kiongozi wa UNHCR Mratibu wa Mazingira idara ya Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Thobias Sijabaje, kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko katika Kikao cha baraza la madiwani kilicho andaliwa na REDESO kwaajili ya kutoa tathimini , kukabidhi fedha na vifaa vya ofisi kwa maafisa wa Maliasili na madiwani kuelimishwa jinsi ya kutoa elimu kwa Wanawake na vijana juu ya utunzaji wa mazingira. 

Alisema  shirika la UNHCR kwa kupitia REDESO limeamua kutoa Vifaa hivyo na mafunzo kwa madiwani kutokana na hali ya uharibifu wa mazingira  ilivyo katika maeneo yanayo zunguka kambi za wakimbizi kutokana na ujio wa wakimbizi uliopelekea athari kubwa iliyopelekea misitu mingi kuharibiwa lengo ikiwa ni kutafuta ufumbuzi juu ya Suala hilo.

"Kwa kuzingatia hilo tumeandaa mpango wa zaidi ya bilioni moja ya uhifadhi wa mazingira ilikuweza kushirikiana na halmashauri katika kutunza misitu , kwakuanzia tumeanza na vifaa ambavyo tumtetoa kwa wataalamu kuweza kufuatilia maeneo yaliyo haribiwa kwa kiasi kikubwa ilikuweza kupanda miti na kutoa elimu ya uhifadh wa mazingira kwa Wananchi",alisema Sijabeje.

Alisema tatizo la mazingira katika kambi za wakimbizi huwa halikwepeki katika vijiji vinavyo zunguka kambi uharibifu Mkubwa umefanyika.Baada ya kuliona tatizo hilo linalo pelekea uharibifu wa  na uongozi wa  UNHCR kuweza kuangalia jinsi gani ya kutatua tatizo hilo,  na kuamua badala ya kutumia kuni na kujenga Nyumba kwa kutumia miti waliamua kubuni njia ya ufyatuaji wa tofari zinazo tumia udongo,chokaa na Simenti pamoja na kutengeneza majiko yenye uwezo wa o tumia kuni kidogo ilikuepukana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira. ya

Athari zilizo sababishwa na ujio wa wakimbizi ni pamoja na uharibifu wa mazingira katika maeneo ya kambi zao na maeneo yaliyo jirani na kambi hiyo, kutokana na ukataji wa miti, uharibifu wa vyanzo vya maji na  kwaajili ya matumizi ya kujengea Nyumba za wakimbizi za kudumu na matumizi ya kuni kwaajili ya kupikia.

Aidha  Mtaalamu wa Mazingira Taifa Dkt Braiton Gwamagobe alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuingia misituni na kukata misitu bila kujali madhala yanayo weza kujitokeza hali inayopelekea ukame na uharibifu wa tabaka la ozoni unaosababishwa na hewa chafu kutokana na kutokuwa na miti ya kutosha.

Gwamagobe alisema  wakitaka elimu ya utunzaji wa misitu na mazingira ifanikiwe ni pamoja na kutoa elimu hiyo kwa Vijana na wanawake ambao ndio watumiaji wakubwa wa maliasili za misitu kutokana na nguvu kazi waliyo nayo  inayopelekea uharibifu wa  miti kwa kuchoma mkaa, ukataji wa mbao na kulima maeneo ya vyanzo vya maji.

Alisema katika utafiti walio ufanya katika Wilaya ya kakonko wamebaini uharibifu Mkubwa umefanyika hasa katika maeneo ya Kambi za wakimbizi na vijiji vinavyo zungika kambi hizo, na baada ya kufanya tathimini walibaini wanao jihusisha na shughuli hizo wengi wao ni vijana ambao wakipatiwa elimu watasaidia kupambana na athari hizo.

Akitoa Shukrani zake wakati akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala aliwashukuru UNHCR kwa kuthamini umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwawezesha maafisa wa maliasili kufanya shughuli za utunzaji wa mazingira na kutoa wito  kwa maafisa hao kuvitumia vifaa hivyo kwa kazi ya utunzaji wa mazingira na si kwa kazi nyingine.

Alisema Vifaa hivyo vitumike kuwapatia elimu Wananchi wa Vijiijini jinsi ya kutunza mazingira ,kuzungukia maeneo ya liyo halibiwa kwa ukataji miti na sio vifaa vya kufanyia Shughuli zao binafsi ilikufikia lengo la uboreshaji wa mazingira kama mkakati wa UNHCR unavyo eleza. 
Posted by MROKI On Tuesday, January 24, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo