Nafasi Ya Matangazo

January 14, 2017

Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.

Katibu Mkuu uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo  ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff  ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.

“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.

Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.

Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji  marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.

Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.

Naye Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu kwani ni urithi wa kila mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huu wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.
Posted by MROKI On Saturday, January 14, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo