Nafasi Ya Matangazo

January 06, 2017

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Simu ya Mkononi mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya wakusanya taarifa za Bei za Mazao ya kilimo na Bidhaa Nyingine ikiwa ni kitendea kazi kitakachowasaidia wakusanya taarifa.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa  tatu kulia)  walioketi kwenye viti akiwa na picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Ukusanyaji wa Taarifa za Bei za Mazao ya Kilimo na Bidhaa Nyingine yanayofanyika Mkoani Dodoma.Wa Pili (Kulia) walioketi ni Bw. Odilo Majengo Mkurugenzi Idara ya Uhamasishaji Biashara na Bi. Hilda Mwampeta Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhamasishaji Biashara na  Masoko Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji.
                                                                ********************

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (WVBU) Prof. Adolf Mkenda amehitimisha mafunzo  ya ukusanyaji wa taarifa za bei za mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kwa kukabidhi simu za Mkononi Washiriki wa Mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara. 

Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani hapa kwa siku nne mfululizo na kuwashirikisha wakusanya taarifa wapatao 113 ngazi ya wilaya na mikoa.

Katika Hotuba yake ya ufunguzi alieleza malengo ya Mafunzo hayo kuwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa weledi zaidi kwa kuzingatia maendeleo ya kiteknologia na Habari kadiri mahitaji ya taarifa yanavyoongezeka. 

“mafunzo haya mnayopatiwa yanalenga kuwawezesha kukusanya na kutuma taarifa za masoko ya mazao ya Kilimo pamoja na bidhaa nyingine kwa wakati na usahihi Zaidi”.

Alisisitiza kuwa taarifa sahihi zitasaidia wakulima,wafanyabiashara, watunga sera na Taasisi  nyingine kufanya mamuzi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi yatakayoongozwa na uchumi wa Viwanda. 

“Ni matumani yangu kuwa mtatumia weledi wenu na uzalendo kuwapatia wakulima, wasindikaji au wenye viwanda na walaji taarifa sahihi watakazozitumia katika kuendesha shughuli za kibiashara”.

Aliongeza kuwa taarifa sahihi na kwa wakati utasaidia kuondoa utitiri wa madalali ambao hutumia mwanya wa ukosefu wa taarifa kuwanyonya  wakulima kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile kwenda moja kwa moja kwa wakulima na kununua mazao  kwa wakulima badala ya kusubiri mazao yafike sokoni.

Mafunzo haya yaliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kupitia  Mradi wa SECO UN TRADE, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) .
Posted by MROKI On Friday, January 06, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo