Nafasi Ya Matangazo

January 26, 2017

 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dr Jim Yonazi (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) Dr Seleman Sewangi wakiweka saini makualiano ya kukuza lugha ya Kiswahili kupitia gazeti la Habarileo. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Mhariri wa TSN, Tuma Abdallah na Kaimu Mhariri wa Gazeti la Habarileo, Nicodemas Ikonko na kulia walioketi n Mwanasheria wa kampuni ya TSN, Mwadawa Ally. 
  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dr Jim Yonazi (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA) Dr Seleman Sewangi, wakibadilishana nyaraka. 
Wafanyakazi wa magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo wakifuatilia matukio katika kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la Habarileo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia) akiteta jambo na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi. 
MHARIRI Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi amesema, gazeti la serikali la lugha ya Kiswahili linaongeza wigo wa serikali kuwasiliana na wananchi na ni daraja muhimu kati ya serikali na wananchi.
DK. Yonazi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya miaka 10 ya gazeti la Habarileo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 
Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete alilizindua gazeti la HabariLeo Desemba 21, mwaka 2006 katika ukumbi wa Chimwaga, Dodoma.
Kwa mujibu wa Dk. Yonazi, gazeti la Habarileo limepewa kazi ya kuhabarisha, kuelimisha , kuburudisha na kuhoji mambo serikalini, katika chama na kwa wananchi.
“Kwa miaka 10 gazeti hili limekuwa likitekeleza wajibu wake katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata taarifa mbalimbali zinazohusu shughuli za serikali na pia kuhoji kwa niaba ya wananchi kuhusu mambo mbalimbali ambayo hayaonekani kwenda vyema serikalini amba katika chama tawala” amesema Dk. Yonazi.
Dk. Yonazi amesema, gazeti hilo limekuwa chachu ya kuibua hoja za maendeleo ya jamii na lwatu wengi wamukwa wakilitumia kwa rejea hasa wasomi na wanaofanya uamuzi katika ngazi za kiutendaji.
“Kama yalivyo magazeti mengine ya TSN, gazeti la Habarileo limekuwa ni nyenzo muhimu ya kuhabarisha na kuelimisha umma juu ya masuala mbalimbali katika nyanja za sayansi, elimu, jamii, siasa, uchumi na utamaduni” amesema katika sherehe hizo kwenye Uwanja wa Taifa .
Dk. Yonazi amesema, Habarileo ni gazeti la kijamii zaidi linalojitofautisha na magazeti mengine na kwamba, msimamo wake unazingatia kuhimiza maendeleo na kuleta matumaini.
“Kazi nyingine muhimu ya gazeti hili ni pamoja na kuanika na kudodosa mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka kuelekea uchumi wa kati na kuwasilisha maoni ya wananchi kuhusiana na mikakati hiyo hasa dira ya mwaka 2025 inayoweka wazi vipaumbele vya serikali” amesema.
Amesema, mitandao ya kijamii ni changamoto kubwa kwa Habarileo kwa kuwa inawezesha wateja wa magazeti kupata habari mapema zaidi kuliko zile za magazeti yanayosomwa siku inayofuata.

“Tayari hatua madhubuti zimeanza kuchukuliwa na kampuni ya TSN kwa kuimarisha kitengo chake cha habari mtandao na kuhakikisha wasomaji wanapata habari kadri zinavyotokea”amesema.
 Meza kuu ikigonganisha glasi kulitakia heri na fanaka gazeti la Habarileo. 
 Wafanyakazi nao wakifurahia 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali na waalikwa maalum wakikata keki. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amkimlisha keki Naibu Mhariri Mtendaji, Tuma Abdallah. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimlisha keki Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonaz. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na 
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonaz wakitoa buruani ya muziki. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipiga gitaa 
 Wafanyakazi wakiserebuka na muziki wakati wa tafrija hiyo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiangalia picha ya ukutani aliyozawadiwa. 
Posted by MROKI On Thursday, January 26, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo