Nafasi Ya Matangazo

January 26, 2017

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sita (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB,Edmund Mkwawa kwa kufanikisha benki hiyo kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao baada ya Meya huyo kuzindua Huduma ya DCB Pesa na DCb jirani juzi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sita, (kulia) akipeperusha bendera na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka kuashiria uzinduzi wa huduma za DCB Pesa na DCB Jirani.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sita (katikati) akizindua huduma za DCB Pesa na DCB Jirani  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB,Edmund Mkwawa kwa kufanikisha benki hiyo kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao baada ya Meya huyo kuzindua Huduma ya DCB Pesa na DCb jirani juzi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitaakimkabidhi zawadi ya simu mshindi wa bahati nasibu ya Benki ya DCB, Stoph Sanga.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sita amkimabidhi zawadi Joyce Willson aliyepokea zawadi ya ada ya shule kwa niaba ya mtoto wake Josephine Willson aliyeshinda kupitia akaunti maalum ya Watoto.
 Mmoja wa washindi 10 wa fulana akipokea zawadi yake kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB,Edmund Mkwawa akizungumza na kusema kuwa Huduma ya DCB Jirani itaisaidia kwa kiasi kikubwa benki hiyo kuongeza idadi ya wateja kwa kufikisha huduma za kibenki kwa watu walio mbali na mijini. 

Alisema Benki pia kupitia huduma hiyo itapunguza gharama za ujenzi wa matawi, kusaidia benki kupata amana za kutosha ambazo ndio uti wa mgongo wa Benki yeyote duniani na kuongeza gawio kwa wahudumu wake.

DCB itatumia mashine zao wenyewe kutoa huduma hiyo ambapo alisema huduma itamuwezesha mteja kuweka, kutoa na kuhamisha fedha na kulipia bili.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka akizungumza na kusema kuwa Benki inaendelea na mikakati yake ya kubunina kuanzisha huduma za kisasa zinazoendana na ukuaji wa teknolojia ulimwenguni, lengo likiwa kumuwezesha mteja kuzipata kwa urahisi zaidi.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sita (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB,Edmund Mkwawa kwa kufanikisha benki hiyo kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao
 Meza kuu ikifuatilia matukio.
 Watumishi mbalimbali wa Benki ya DCB wakiwa katika tukio hilo.
 Wateja waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.
Posted by MROKI On Thursday, January 26, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo