Nafasi Ya Matangazo

January 27, 2017

 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza wakati alipoongoza kamati ya ulinzi na Usalama wilayani humo kuzungumza na majirani zao waa Wilaya ya Mabanda mkoa wa Makamba nchini Burundi.
 Kanali Gaguti akizungumza.
 Ziara ikiendelea...
Na FK Blog Kigoma,
MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma Kanali Marco Gaguti amewaonya waomba hifadhi wenye historia ya uhalifu nchini Burundi  wanaoingia Nchini  Tanzania kwa kigezo cha kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa kuhofia wasikamatwe kwa uhalifu walioufanya Nchini mwao kuwa ikibainika  hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha, Gaguti aliuomba uongozi wa Nchi ya Burundi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya   Wilaya hiyo iliyopo Mpakani, kuweza kuwabaini waomba hifadhi wanaoingia Nchini kwa kukimbia uhalifu walioufanya Nchini mwao na kuja kuendeleza vitendo hivyo wanapo ingia Nchini.

Hayo yalibainika jana wakati wa Kikao cha majadiliano baina ya Mkuu huyo na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, alipokuwa akihoji ni kwanini wahamiaji wengi wanaongezeka Nchini wakidai wanakimbia vurugu zinazo endelea Nchini mwao ambapo kwa Mwezi january  waliingia waomba hifadhi 2230, ambapo ilibainika wengi wao wanadai wanakimbia kukamatwa kwa kujihusisha na uhalifu na wengine kukimbia njaa iliyopo majumbani kwao.

Gaguti alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji wanaoingia Nchini wakidai kukimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha Vijana wa chama tawala kinacho julikana kama  ( IMBONELAKULE)  ambapo wanakuja kuomba hifadhi katika Nchi ya Tanzania ilihali Nchi yao inaamani ya kutosha  na wengine kukimbilia kambini kuweza kupata hufuma za bure kwa kuhofia njaa nchini mwao . Hali iliyopelekea Waziri wa Mambo ya ndani kusitisha zoezi la Waomba hifadhi kuingia Nchini kwa kigezo cha kukimbia njaa Nchini mwao na kukimbilia Tanzania iliwaweze kupata Msaada wa chakula , ni lazima Afanyiwe mahojiano na atoe sababu zilizo mfanya akimbie iliaweze kupatiwa kibali cha kuwa mkimbizi.

Hata hivyo Kanali Gaguti aliwaomba viongozi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuweza kuwabaini wahalifu hao waweze kurudisha Nchini mwao na kuweza kuepukana na vitendo vinavyo endelea na ongezeko la waomba hifadhi kuingia Nchini bila kufuata utaratibu.

'' leo nilikuwa natembelea vituo na kuona ongezeko ya wahamiaji lakini serikali imetoa maelekezo mpya ikiwemo kuwatambua na kujua sababu za kukimbia Nchini mwao lakini kama atakuwa na sababu za Msingi hata pata fursa ya kuwa mkimbizi, lakini pia nikuombe ushirikiano kama kuna taarifa za watu ambao ni wahalifu upewe taarifa mape ma kabla ya mambo kubadilika Ile tuweze kuchukua tahadhari mape ma kwa panda zote mbili" alisema kanali Gaguti.

Naye mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba (Musitanteri)Niyonkuru Laetitia alisema kwa sasa nchi ya Burundi ni tulivu na wanaokimbia nchini  mwao ni wale wanaokimbia njaa na wengine kukimbia uhalifu aliofanya nchini Burundi na kuja Tanzania kuomba hifadhi.

Alisema wengi waliofika Tanzania ni wale waliokimbia kwa mambo yao binafsi na wengine ni wale wakimbizi waliorudishwa BUrundi kipindi cha nyuma wanaokimbia wengi wanakuja kwa kigezo cha kupelekwa nje ya Nchi kama vile America na Ulayana Nchi nyingine ilikuwafuata ndugu zao walio pelekwa huko .  

Aidha aliuomba Uongozi wa Tanzania kabla ya kuwapokea wahamiahi hao kuchukua vitambulisho vyao ilikubaini walio kimbia tuhuma zinazo wakabili, pia kumekuwa na tetesi wengi wao wanaoingia kuomba hifadhi wanakuja makambini kujifunza namna wanavyo weza kwenda kuipindua Nchi kwa kupigana pindi wanapo wabaini waweze kuwakabidhi kwa Serikali ya Burundi.

Kwa upande wao baadhi ya Waomba hifadhi waliofika katika maeneo ya kupokelea waomba hifadhi hao kwa mahojiano waweze kuingia kambini ,wengi wao walidai wanakimbia vikundi vya IMBONELAKULE vinavyo wafuata Nyumbani kwao usiku na kuwapiga na kuwatishia usalama wao hali inayo walazimu kukimbilia Tanzania , suala lililo kanushwa na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda.

Nizigimana Silivesta ni moja kati ya  waomba hifadhi kutoka Burundi, alisema kinacho wapelekea kukimbia Nchini mwao ni hali ya kiusalama kuwa ndogo kumekuwa na tabia ya vikundi vya watu vinavyo wafuata kuwatisha kutokana na baadhi ya ndugu zao walio kimbilia nchini kuwa wanamahusiano nao na wanaipinga serikali.
Posted by MROKI On Friday, January 27, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo