Nafasi Ya Matangazo

December 07, 2016


Na Father Kidevu Blog - Kigoma,
JUMLA ya miche 200,000 ya miti imetolewa na Shirika la Kuwahudumia wakimbizi UNHCR  Wilayani Kakonko itakayo fidia uharibifu wa mazingira uliofanywa naWakimbizi waliopo katika kambi ya mtendeli kutokana na ukataji wa miti hovyo kwaajili ya kujipatia kuni na miti ya kujengea nyumba za makazi ya kudumu.


Akizungumza na mwandishi wetu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala alisema ujio wa wakimbizi wilayani humo umesababisha uharibifu  mkubwa wa mazingira katika maendeo yanayo izunguka kambi hali inayo weza kupelekea mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mvua katika Wilaya hiyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Ndagala alisema baada ya kuona tatizo hilo nilizungumza na uongozi wa  UNHCR ambao waliahidi kulitatua tatizo hilo na kwasasa wameanza kwa kutoa miche laki mbili ambayo itagawiwa katika vijiji vinavyo izunguka kambi hiyo ilikufidia uharibifu ulio fanyika na kuweza kuweka mazingira vizuri na kuepukana na ukame unaoweza kujitokeza baada ya miti kukosena.

Alisema wakimbizi wamekuwa na tabia ya kuingia vijijini na kukata miti  kuichuna iliikauke kwaajili ya kuchukua kuni na miti ya kujengea nyumba za kudumu hali ambayo imepelekea maeneo hayo kubaki bila kuwa na miti .
Aidha Ndagala aliwaomba watumishi wanao wasimamia wakimbizi kuwapatia  miche na wao waweze kupanda miti katika kambi hiyo ilikuweza kupata mazingira safi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa sasa maeneo mengi hayana mvua kutokana na maeneo hayo kukosa uangalizi na wananchi wengi kukata miti hovyo.

Pia mkuu huyo ameliomba shirika linalo hudumia wakimbizi kutoa njia mbadala kwa wakimbizi kwa kuwapa majiko ya gesi au majiko banifu yanayoweza kupunguza utumiaji wa kuni unaopelekea uharibifu wa miti kwa kutumia kuni nyingi katika kupikia.

"Kambi hii ya mtendeli inawakimbizi zaidi ya elfu hamsini endapo wote watategemea kuni kutoka kwa wananchi wetu hali hii inaweza kupelekea uharibofu mkubwa,wengine wamekuwa na tabia ya kuuchuna mti kwenye ngozi na kuupaka chumvi baada ya muda unakauka iliwaweze kuukata kiurahisi endapo watapatiwa njiambadala ya nishati ya kupikia itasaidia kupunguza uharibifu huo",alisema ndagala.


Kwa upande wake Mkuu wa kambi ya mtendeli Inocent Mwaka alisema shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR imeandaa utaratibu wa kutoa majiko banifu yanayo tumia kuni chache wakati wa kupikia ilikuweza kuzuia uharibifu huo na kuweza kuacha mazingira yakiwa salama.

Alisema katika kufidia uharibifu huo kuna miche mingi ina inaoteshwa katika kambi na kugawa kwa Wananchi wanao ishi jirani na kambi na kuiotesha ilikuweza kuepukana na madhara ya uchafuzi wa hali ya hewa na  mabadiliko ya hali  ya tabia ya Nchi.
Posted by MROKI On Wednesday, December 07, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo