Nafasi Ya Matangazo

December 21, 2016


Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya semina ya siku moja ya madalali wa Bima iliyolenga kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) katika Bima.


Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Bima Tanzania Mohamed Jaffer akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam baada ya semina ya siku moja ya madalali wa Bima na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  iliyolenga kuwaelimisha kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwa sekta za Bima.

 ******************
 Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo ya siku moja kwa Madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuifahamu vema Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili waweze kushiriki vema na kuondoa kasoro katika ulipaji wa Kodi ya ongezeko la Thamani kutoka Sekta ya Bima.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla wakati wa mkutano waandishi wa habri kwenye semina ya siku moja kwa Madalali wa Bima( Insurance Brokers) ya kuwajengea uwezo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Alisema kuwa mafunzo hayo yamewaelimisha wanachama hao juu ya Kodi ya zuio , utoaji wa kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) na jinsi ya kulipa kwa njia ya mtandao(Revenue gateway system).

Alisema kuwa TRA imekuwa ikitoa mafunzo hayo kwa Wanachama na Mawakala wa Bima kwa sababu kabla ya Sheria ya Mwaka 2014 walikuwa halipi Kodi na hivyo semina hiyo imesaidia wanachama hao kuwa na uelewa mpana juu ya ulipajji wa kodi ya ongezeko la thamani.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Bima Tanzania Mohamed Jaffer aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa hatua yake ya kutoa elimu kwa wanachama wake kwani imesaidia sana kuwajengea uwezo ambao utasaidia ulipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani.

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa makosa katika masuala ya ulipajji kodi na jinsi ya ujazaji wa malipo ya kodi kwa wanachama wao.

Jaffer alisema kuwa ni muhimu sana wanachama wa Chama chake kuelewa vema jinsi ya kujaza na kulipa kodi kwani asilimia 60 ya mapato ya Bima yanatokana na madalali wa Bima kwa kuwa wao ndio wako karibu na wateja kuliko Kampuni za Bima ambazo zinabaki na asilimia 40.

Alisema kuwa hadi hivi Chama hicho kina wanachama wapato 150 ambao wamesambaa Nchi nzima ambao kwa mwaka uliopita waliweza kukusanya wastani wa shilingi bilioni 370.

Kati ya fedha hizo asilimia 18 ndio ulipwa kodi ya ongezeko la thamani na kuongeza kuwa kiwango cha makusanyo kwa mwaka huu kinatarajjiwa kuongeza na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya VAT.
Posted by MROKI On Wednesday, December 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo