Nafasi Ya Matangazo

December 24, 2016MTUMISHI wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Modest Mfutakamba Mfilinge (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.

Kufuatia msiba huo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemtumia salamu za rambirambi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na familia ya Mfilinge kufuatia kifo hicho.

Aidha Waziri Nape ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku kilichotokea Desemba 23,2016 katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam.

Waziri pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.

Waziri Nape amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo na ameeleza kuwa, kifo chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha kwasababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times, The Guardian, Nipashe na Mwananchi na The Citizen.

Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi. Amina.
Posted by MROKI On Saturday, December 24, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo