Nafasi Ya Matangazo

December 27, 2016

Maelfu ya wakazo wa Mji wa Dodoma hususani kutoka Katika maeneo ya Msalato mkoani hapa waliungana na familia ya Bukuku katika kukamilisha safari ya mwisho ya mpendwa wao, Mpoki Bukuku aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian Limited, aliyefariki Desemba 23, 2016 kwa kugongwa na gari katika eneo la ITV Mwenge, jijini Dra es Salaam.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki na kuongoza maziko hayo ya Mwanahabari huyo ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

Pia alikuwepo Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazoro Nyalandu na viongozi wengine mbalimbali wa vyama na serikali wa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde  (kushoto) na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Mpoki Bukuku aliyekuwa Mpigapicha wa Magazeti ya The Guardian aliyefariki hivi karibuni kwa kugongwa na gari na kuzikwa Msalato Dodoma leo.
 Mama Mzazi wa Mpoki Bukuku, akiweka Shada la Maua kwenye kaburi la Mtoto wake.
Mjane wa Mareheu akiweka shada la maua.
 Watoto wa Marehemu wakienda kuweka Shada la Maua kwenye kaburi la baba yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde akizungumza.
 Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu  akizungumza
 Mwakilishi wa The Guardian Ltd, Kanda ya Kati, Daniel Mkate akizungumza.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Magezi  ya Serikali TSN, Arban Epimark akitoa Salamu za Pole.
 Mwakilishi wa Wapigapicha Tanzania, Mroki Mroki 'Father Kidevu' akitoa Salamu kwaniaba ya Wapigapicha. BOFYA HAPA KUOA PICHA ZAIDI.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma, Habel Chidawali akitoa salamu kwa niaba ya waandishi wa Dodoma.
Mwakilishi wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), John Bukuku akitoa salamu za Bloggers.
 Muda wa kutoa heshima za mwisho ulifika na watu mbalimbali walitoa heshima za mwisho.
 Mkurugenzi wa CDA Dodoma nae akitoa heshima.
 MC Maarufu wa Shughuli za Serikali, Mavunde nae alikuwepo.

Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kutoa heshima
 Viongozi wa Dini wakiwa katika msiba huo wa Mpoki Bukuku
 Mama Mzazi wa Mpoki (kushoto) na Mke wa Marehemu (kulia) wakiwa jirani na jeneza la mpendwa wao.
 Familia ya Marehemu ikiongozwa na Mkewe ikitoa heshima za mwisho.
 Mama akifarijiwa na mwana familia.
 Mke wa marehemu akiaga wakati mwili ukishushwa kaburuni, huku kitinda mimba wa marehemu akiangalia.
 Huyu ni swahiba wa marehemu Mpoki Bukuku kutoka Pale Mtaani Tabata Kimanaga Bwawani
 Jeneza likiwekwa sawa kabla ya kushushwa
 Mjaomba wa Marehemu akilia kwa uchungu.
 Vijana wakifukia kaburi hilo.
Ufukiaji ukielekea kukamilika 
 wanafamilia katika picha baada ya mazishi.
Familia ya marehemu nayo ilipiga picha.
Posted by MROKI On Tuesday, December 27, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo