Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2016



Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Kanali Marko Gaguti akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Munanila, Wilayani humo katika siku yake ya kwanza ya kutembelea kaya kaya 307 zilizo andikishwakunufaika kupitia mfuko wa TASAF kusaidia kaya masikini.
 Kanali Gaguti akiendelea na ziara yake.

 Hapa ni kama mhusika hakuwepo nyumbani.
 Kanali Gaguti akizungumza na mmoja wa nufaika.
Na Father Kidevu Blog- Buhigwe
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti ameanza ziara ya siku 10 ya kutembelea nyumba kwa nyumba  ilikuweza kuwabaini watu wanaonufaika na mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF  awamu ya tatu  ambao hawana sifa ya kunufaika na mpango huo waweze kuondolewa.

Katika ziara hiyo iliyoanza jana katika Kijiji cha Munanila alisema katika Wilaya ya Buhigwe kuna jumla ya kaya 307 zilizo andikishwa kama kaya masikini lakini hazina vigezo vya kunufaika na mradi huu kutokana na hali zao za kiuchumi na mazingira  wanayo ishi hayaonyeshi kuwa ni masikini hivyo watatakiwa kuondolewa katika mpango huo.

Alisema Ziara hiyo itafanyika kwa siku kumi itahusisha viongozi wote wa ngazi ya Kijiji,kata na Wilaya ilikuweza kuwabaini wale wote ambao hawastahili nyumba kwa nyumba ili waondolewe na wanufaika wabaki kuwa wale wanao stahili tuu kupatiwa msaada huo wa kaya lengwa.

Gaguti alisema kunabaadhi ya wanufaika wamekimbia baada ya kupewa taarifa ya uhakiki wa wanufaika wa mradi huo  kwa kuhofia wanaweza kutolewa kwa wale ambao hawakuwepo kwenye kaya zao ilikuweza kuhakikiwa watakuwa wamejiondoa,kwa sasa tumetoa maelekezo kwa viongozi wa vijiji kushirikiana na serikali ilikukamilisha suala hilo kwa nakini bila kumpendelea wala kumuonea mtu yeyote.

"Leo tumeanza zoezi la kuwabaini wanufaika wasio na sifa zoezi hili litakuwa ni la siku kumi katika ziara ya leo tumeweza kuwabaini baadhi ya wanufaika hawana sifa watatakiwa kuondolewa kwenye mradi na kwa waliokwepa kufanyiwa tathimini ya kunufaika na mradi watakuwa wamejiondoa wenyewe tunahitaji kubaki na watu ambao wanasifa ya kupatiwa fedha za TASAF ili lengo la serikali la kuzisaidia kaya masikini litimie",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Buhigwe Chubwa Deogratius alisema mkakati wa kuwaingiza wahusika ulishirikisha jamii husika pamoja na wenyeviti wa vijiji ambapo Wananchi wenyewe walikuwa wakidangsnya taarifa yupi anastahili kuingizwa kwenye mpango na yupi hastahili .

Alisema baada ya kupokea barua kutoka Wizarali sisi kama wasimamizi wa mpango huu tumeamua kupita nyumba kwa nyumba kwa walengwa ilikuweza kujilizisha yupi anastahili kuendelea kuingizwa kwenye mpango na yupi hastahili ilikuweza kukamilisha adhima ya serikali ya kuzisaidia kaya masikini.

Katika ziara ya siku ya leo kuna jumla ya kaya tatu ambazo hazina sifa. Anjelina Josia na Veronica James ni baadhi ya wanufaika walio kuwa  kwenye mpango na hawana vigezo vya kuwemo kwenye mpango huo wakati kuna baadhi wenye vigezo vya kuwa kaya masikini wameshindwa kuingizwa kwenye mpango hali ambayo inatia wasiwasi  na ziara hiyo kuendelea na uchunguzi. 
Posted by MROKI On Thursday, December 08, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo