Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2016

 Kiwanda cha Akberalis Hardware & Electric Ltd ni miongoni mwa viwanda vilivyopo nchini Tanzania kinachozalisha kamba za Manila za ukubwa wa aina mbalimbali. Kiwanda hicho ndio wazalishaji wa kamba hizo za manila za Dar Ropes na nimiongoni mwa viwanda vilivyoshiriki maonesho ya mwaka huu ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa yanapofanyika Maonesho ya kila mwaka ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu sabasaba.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Edwin Rutageruka akiangalia kamba za manila za Dar Ropes zinazozalishwa na Kiwanda cha Akberalis kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Viwanda vya ndani katika uwanja wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa jana. Kushoto ni Meneja Masoko Ricky Sadick na Meneja wa Kiwanda hicho Yona Kibaso.
 Wakazi wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini wanaoingia ndani ya Banda la Karume wanafika katika banda la Dar Ropes kujipatia maelezo juu ya kamba hizo imara na bora.
 Meneja wa Kiwanda hicho Yona Kibaso ni miongoni mwa waofisa wa juu wa kiwanda hicho waliopo katika banda kuhudumia wateja.
 Meneja Masoko Ricky Sadick akizungumza na waandishi wa habari. 
  Meneja Masoko Ricky Sadickakihudumia wateja.
 Tabasamu ni moja ya mapokezi utakayoyapata ukifika katika banda la DAR ROPES
Meneja Masoko Ricky Sadickakihudumia wateja.
Posted by MROKI On Thursday, December 08, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo