Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2016


Meneja Mwandamizi Mikakati na Ubunifu wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati Benki hioyo ikitangaza promotion maalum kwa wateja wapya na wazamani wa benki hiyo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shughuli za kibenki, Haika Machaku na kushoto ni Meneja Masoko wa Benki ya DCB, Boyd Mwaisame.
Meneja Mwandamizi Mikakati na Ubunifu wa Benki ya DCB, Samwel Dyamo (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati Benki hioyo ikitangaza promotion maalum kwa wateja wapya na wazamani wa benki hiyo Dar es Salaam jana
***************
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KAMPENI YA KUWEKA AMANA DCB BENKI INAYOITWA ‘BORESHA MAISHA NA DCB, PATA FAIDA NA DCB’

DCB Commercial Bank, iliyo anza kutoa huduma kwa wateja miaka 14 iliyopita sasa inawaletea wateja wake kampeni maalum inayoitwa ‘Boresha Maisha na DCB, Pata Faida na DCB’ kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Novemba 28 mwaka huu hadi 29 Februari 2017.

Kampeni ya Boresha maisha na DCB inalenga kunufaisha kwa kutoa zawadi kwa wateja wetu wapya na wa zamani, baada ya kuweka pesa mara kwa mara kwenye akaunti mojawapo ya Akiba binafsi, akaunti ya watoto na akaunti ya WAHI kiasi cha kuanzia shi. 50,000 na kuendelea na kuongeza amana kwenye akaunti zao mara mbili zaidi ya Shi. 500,000. Mteja huyu atapata nafasi ya kuingia kwenye draw ya bahati nasibu itakayochezeshwa kila mwezi na kujishindia Tshirt, simu za mkononi au pesa taslimu shi. 200,000 kwa ajili ya ada ya mtoto shule. 

Tunatarajia kuchezesha draw tatu za bahati nasibu, draw ya kwanza itachezwa tarehe 17 Disemba 2016, ya pili tarehe 17 Januari 2017 na ya mwisho itachezwa tarehe 17 Februari 2017. Washindi watataarifiwa mara moja baada ya kushinda mbele ya waandishi wa habari na ili kuwatambua watatakiwa kuwasilisha vitambulisho vyao wakati wa kuchukua zawadi zao mojawapo ya vifuatavyo; leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura au kitambulisha cha utaifa. 

Idadi ya washindi kwa kila draw ya bahati nasibu  itakuwa kama ifuatavyo:
i.             Washindi wa Tshirts watakuwa - 20
ii.            Washindi wa simu za mkononi -  2
iii.           Washindi wa pesa taslimum kwa ajili ya ada shule - 3.

Pata faida na DCB ni kampeni inayowapa faida kubwa wateja wetu kwa kuwekeza na DCB kupitia huduma yetu ya Akaunti ya muda maalumu. Kwa wateja wetu watakao wekeza DCB kiasi cha shi. Milioni 50 na kuendelea kwa muda wa kuanzia mwaka mmoja watapata faida kubwa ya hadi asilimia 15 na kuendelea kutegemeana na Ukubwa wa amana zake.

Tunatoa wito kwa wateja wetu na wasio wateja,  watu binafsi, wajasiriamali na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hili na kufaidika. Kadhalika tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma bora kutoka DCB Commecial Bank. Tunawaahidi tutaendelea kuboresha zaidi huduma zetu ili muendelee kufaidika nazo kupitia kampeni hii ya Boresha maisha na DCB, Faidika na DCB.
Posted by MROKI On Thursday, December 08, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo