Nafasi Ya Matangazo

November 24, 2016

 Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) Dk Judith Odunga akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusiana na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia nchini utakaofanyika kuanzia Novemba 25-Desemba 10 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Rennie Godwe na kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake na Watoto nchini (TWCWC), Edda Mariki.
 Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) Dk Judith Odunga akizungumza
 Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) Dk Judith Odunga akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusiana na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia nchini utakaofanyika kuanzia Novemba 25-Desemba 10 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Rennie Godwe
 Wadau wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wakifuatilia taarifa hiyo.
 Wadau walisikiliza kwa makini BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 Mmoja wa waratibu akizungumzia maadhimisho hayo.
Afisa wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi wa Ilala Christina Onyangona Mratibu wa matembezi hayo akitoa takwimu za makosa yaliyoripotiwa na kufikishwa Mahakamani na kutolewa uamuzi. 
**************
MASHIRIKA yanayopambana na ukatatili wa kijinsia yanatarajia kuathimisha siku 16 kupinga ukatili huo sambamba na kujenga uelewa kwa umma.

Shirika  hayo ni Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Shirika la Kimataifa la Wanawake (UN-Women) pamoja na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,  Mkurugenzi wa WiLDAF Dk Judith  Odunga maadhimisho hayo yanatarajia kuanza Novemba 25 na kufikia kilele chake Desemba 10 mwaka huu.

"Maadhimisho hayo yana lengo la kutoa elimu na kuhamasisha Umma kupinga ukatili wa kijinsia na kuhimiza umuhimu wa elimu salama kwa wote," alisema Dk Odunga.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angelah Kairuki.

Alisema Novemba 29 mwaka huu ni siku ya kimataifa ya watetezi wa Haki za Binadamu wakati Desemba 1 ni siku ya Ukimwi Duniani.

Alisema kuwa siku nyingine muhimu kwa mwezi ujao ni Desemba 3 ambayo ni siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu na waakati Desemba 6 ni siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ya Montreal 1989 ambapo wanawake 14 waliuwawa na mtu aliyekuwa anawachukia wanawake.

Odunga alisema "siku hizo 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni tukio la kimataifa la kila mwaka ambalo lina lengo la  kuwa na nguvu  ya pamoja katika kuzuia  kuenea kwa janga hilo, ambapo hapa nchini utafanyika katika kanda tano," alisema.

Alisitaja kanda hizo kuwa ni Kanda ya Mashariki na Dar es Salaam, Kanda ya Kati Dodoma, Kaskazini, Kusini na Kanda ya ziwa na katika kila kanda kutakuwa na shughuli mbalimbali kama vile midahalo ambayo italeta chachu ya mabadiliko katika nchi pamoja na  maandamano ya amani.

Afisa wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi wa Ilala Christina Onyango amesema kuwa maadhimisho hayo yamesaidia kuongeza uelewa kwa jamii , hatua ambayo imesaidia kupokelewa kwa kesi nyingi za ubakaji ukilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Mwaka jana Ilala ilipokea kesi 216 za ubakaji na kati ya  kesi hizo,  25  zilifikia hukumu kutokana na kukosa ushahidi tu, lakini kwa mwaka huu kesi 226 zilipokelewa na 112 zilipata hukumu, baada ya jamii kuelimika hivyo kutoa ushirikiano mzuri katika ushahidi” alisema Onyango.

Kauli mbiu ya maadhinmisho ya mwaka huu ni funguka pinga ukatii wa kijinsia,  elimu salama kwa wote.
Posted by MROKI On Thursday, November 24, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo