Nafasi Ya Matangazo

November 09, 2016

SHIRIKA la Ndege la Kitanzania, Precision Air, limezindua promosheni maalmu kwa ajili ya kuwazawadia wateja wake kuelekea msimu wa sikukuu. Promosheni hiyo iliyopewa jina la SAFIRI NA USHINDE  imezinduliwa jana kupitia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya shirika hilo.

 Kupitia promosheni hiyo tiketi 100 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni hiyo. Tiketi hizo zitatolewa kupitia droo zitakazochezeshwa kila wiki kwa wiki kumi mfululizo, na washindi watajipatia tiketi ya bure kusafiria kwenda popote ndani ya mtandao wa Precision Air.

Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja Masoko na Mawasiliano Bi. Azda Nkullo amesema, kila abiria na mteja ana nafasi ya kushinda tiketi ya bure ilimradi tu amesafiri na Precision Air. 

 “Tunasherekea miaka 23 ya kutoa huduma, na katika kufanya hivyo tutatoa tiketi hizi 100 bure kwa wateja wetu, kama mkono wa shukrani kwa kuwa pamoja nasi kwa kipindi chote ambacho tumekua tukitoa huduma.” Aliongeza Bi. Nkullo

Bi. Nkullo ameleza kuwa kwa mteja kushiriki katiko promosheni hii, anahitajika kununua tiketi ya Precision Air kwenda popote kule ndani ya mtando wake na kasha kujaza kuponi ya ushiriki wakati wakujisajili na safari na kuikabidhi kwa muhudumu wakati wakuanza safari. 

Tutafanya droo kila Jumatatu ya wiki kwa wiki kumi mfululizo na kuwatangaza washindi wetu 10 kila wiki. Tunawasihii wateja wetu kuchangamkia fursaa hii ya kujipatia tiketi ya bure kupitia promosheni hii hasa katika wakati huu ambapo wanajiandaa na msimu wa sikukuu. Amesisitiz Bi.Nkullo.

Kwa upande wake Meneja Uratibu na Mahusiano Bw. Hillary Mremi amesema wateja wanaweza kushiriki promosheni hi kwa urahisi kwa kuchangamkia tiketi za promosheni kupitia tovuti ya Precision Air maarufu kama shavu la dotcom kwa safari kati ya Dar-Arusha, Dar-Kilimanjaro, Musoma-Mwanza and Mwanza-Bukoba kwa nauli inayoanzia Sh. 80,000/- 

Bw. Hillary Mremi ameongeza pia kuwa tiketi zote zitakazo nunuliwa kupitia tovuti ya Precision Air zitakua na punguzo la asilimia 10 (10%).

 Precision Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, ikitumia ndege ndogo ibebayo abiria wa tano aina Piper Aztec. Katika kuanza kwake Precision Air ilikua imejikita katika kusafirisha watalii waliokua wakitembelea vivutio vya utalii nchini (Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar) huku makao makuu yake yakiwa Arusha.

Ikiwa ni miaka 23 ya Precision Air kutoa huduma, Shirika la ndege la Precision Air limekua na kua moja ya mashirika ya ndege ya nayoheshimika Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani kuelekea sehemu 11 na safari 2 za kikanda, likiunganisha abiria kuelekea maeneo mengi zaidi ndani ya Africa na kimataifa.
Posted by MROKI On Wednesday, November 09, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo