Nafasi Ya Matangazo

November 10, 2016Bety Alex,FK Blog-Arusha
Ajali za pikipiki kwa mkoa wa arusha zimeongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 zilifika ajali 836 huku upande ajali za magari zikipungua kwa asilimia 11.

Hataivyo ajali hizo za pikipiki kwa mwaka 2010 zilikuwa 709 ukilinganisha na ajali 277 za pikipiki mwaka 2009 ajali hizo za pikipiki bado zinaendelea kuongezeka.

Hayo yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani wakati akielezea hali ya usalama wa barabarani kwenye uzinduzi wa maazimisho ya wiki ya usalama barabarani  mapema leo.

Selemani alisema kuwa takwimu zinaonesha mkoa wa Arusha bado unakabiliwa na ajali za barabarani ambapo kwa kipindi cha mwaka 2007 ajali zimekuwa zikiongezeka na kulikuwa na ajali 1807na kufikiakiwango cha juu mwaka 2010 ambapo ajali 2658 huku kwa kipindi cha mwaka 2012 ajali zilianza kupungua hadi kufikia ajali 2011

Alifafanua kuwa baada ya jeshi kutumia nguvu kubwa sana katika kupunguza ajali zinazotokana na magari zilipungua sana ingawaje kwa sasa bado wimbi kubwa la ajali linatokana na ajali za pikipiki.

Katika hatua nyingine alisema kuwa ajali zinasababishwa na sababu za kibinadamu kwa asilimia 75,madereva kulewa huku wakiwa wanaendesha vyombo vya moto,pia ubovu wa vyombo vya usafiri kwa asilimia 15,miundombinu ya barabara kwa asilimia10.

Awali mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya arusha Fabian Daqaro alisema jukumu la usalama wa barabarani sio la polisi wenyewe wala kamati ya kikosi cha usalama barabarani pekee bali ni ulinzi wa kila mtu.

Fabian alisema kuwa endapo kama kila mtu atafuata sheria na kanuni za barabarani basi ajali zitakuwepo kwa kiwango cha asilimia 0.0 kwani ajali zinachangia kudidimiza mlengo wa taifa.

Hataivyo katika uzinduzi huo baadhi ya askari wa usalama barabarani walifanikiwa kupewa vyeti vya ufanyakazi bora ambapo mmoja wa askari hao Silas Konga alisema kuwa maadili yao bora kazini yamechangia wao kutambulika na jeshi hilo.
Posted by MROKI On Thursday, November 10, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo