Nafasi Ya Matangazo

October 13, 2016

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawaarifu walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwamba imeongeza muda wa kuhakiki na kuboresha taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Kwa hiyo uhakiki wa TIN utaendelea hadi tarehe 30 Novemba 2016 hivyo wananchi wote wenye TIN- katika Mkoa wa Dar es Salaam  wanatakiwa kufika katika vituo vilivyoainishwa ili kuboresha na kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe ya mwisho kwa maana muda hautaongezwa tena.

Wale wote watakaoshindwa kuhakiki au kuboresha taarifa zao, TIN zao za zamani zitafungwa na kuondolewa kwenye mfumo hivyo hawataweza tena kutumia namba hizo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA ZOEZI LA UHAKIKI
Wenye TIN za biashara wanatakiwa kuboresha au kuhakiki  taarifa katika ofisi za Mikoa ya kodi ziliposajiliwa biashara zao katika vituo vifuatavyo:-

  • Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
  • Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta)
  • Mkoa wa Kodi Temeke:Uwanja wa Taifa 
  • Ofisi za TRA Kigamboni
  • Ofisi za TRA Mbagala
Wenye TIN zisizo za biashara wanaweza kuboresha au kuhakiki  taarifa zao katika ofisi yoyote ya TRA ya Mkoa au wilaya iliyo karibu nae.  

Fomu za kujiandikisha au kuhakiki  taarifa zinapatikana ofisi zote za TRA na kwenye Tovuti yetu  www.tra.go.tz na zinaweza kujazwa na kuwasilishwa kwa mkono katika vituo vya uhakiki  zikiwa na viambatisho vifuatavyo:

Kitambulisho (Kitambulisho cha kupigia kura au cha taifa, au leseni ya udereva)
Mkataba wa pango au leseni ya Makazi kama unamiliki jengo la biashara.
Cheti cha kuandikishwa cha Kampuni kutoka BRELLA (Certificate of Incorporation)- Kwa Makampuni tu.

Nyaraka za muundo na dhumuni la uanzishwaji wa kampuni(Memorandum and Article of Association)-Kwa Makampuni tu
Cheti cha TIN. 

Mlipakodi atatakiwa kufika yeye mwenyewe ili kuhakiki alama za vidole zilizo kwenye mfumo.

Huduma hii ya uhakiki wa taarifa za mlipakodi inatolewa bila malipo.
Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800780078 / 0800750075 au tuandikie kupitia huduma@tra.go.tz

‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu
Posted by MROKI On Thursday, October 13, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo