Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2016

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata akikata utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa ofisi mpya ya TRA iliyoko Kimara Mwisho leo Oktoba 26, 2016, Kushoto kwake ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya pamoja na Wakurugenzi wengine wa TRA wakishuhudia tukio hilo
Meneja wa TRA Kinondoni, Wallace Mnkande (anayeongea kwa vitendo) akitoa maelezo ya kituo hicho kipya kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata (aliyeketi) wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo. Wengine kutoka kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani, Abdul Zuberi, Meneja wa Majengo Gerald Mwikuka, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu,  Gerald Mwanilwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi,  Richard Kayombo.

Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya akimweleza jambo Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alipotembelea ofisi mpya za TRA Kimara Mwisho kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo.
Meneja wa TRA Kinondoni, Wallace Mnkande akimwonesha jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata (kushoto kwake) alipotembelea ofisi ya TRA Kimara Mwisho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2016



Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata akisalimiana na baadhi ya walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA iliyoko eneo la Kimara Mwisho ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.



Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) , Alphayo Kidata akiongea  na baadhi ya walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA-Kimara Mwisho ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.



Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata – (Mwenye suti ya bluu katikati) pamoja na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA , Elijah Mwandumbya (Kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na walipakodi waliofika katika Ofisi Mpya ya TRA Kimara ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN. Ofisi hiyo imezinduliwa leo tarehe 26 Oktoba 2016 na Kamishna Mkuu wa TRA ili kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi na kuboresha huduma mbalimbali za Kodi.
*******************
KATIKA jitihada za kuboresha huduma kwa walipakodi  na kuzifikisha huduma hizo kwa  karibu zaidi   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata  amezindua ofisi mpya ya TRA katika  eneo la Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam leo.

Ofisi hiyo itatoa huduma zote za kikodi ikiwemo  usajili na uhakiki wa  Namba za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN, Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT, Malipo ya Kodi za Magari, Kodi zote za Mapato zikiwemo Kodi za Makampuni, Watu Binafsi, Wafanyakazi (PAYE), Kuendeleza Ufundi Stadi - SDL, VAT, Ushuru wa Stampu na huduma nyingine za kikodi.


Akizungumza na walipakodi waliofika katika ofisi hiyo kupata huduma wakati wa uzinduzi, Bw. Kidata aliwashukuru kwa mwitikio wao katika zoezi la uhakiki wa taarifa za TIN ambao utaisaidia Mamlaka kupata idadi sahihi ya walipakodi ili kuondoa walipakodi hewa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ulipaji kodi.

“Zoezi hili litaongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi na ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu” Alisema Kidata

Kamishna Mkuu wa TRA aliwataka walipakodi hao wanaoishi maeneo ya karibu na ofisi hiyo mpya ya TRA iliyopo Kimara Mwisho kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma mbalimbali za kikodi ikiwemo uhakiki wa taarifa zao TIN kabla ya tarehe ya mwisho wa zoezi hilo kwa Mkoa wa Dar es Salaam  ambayo ni tarehe  30 Novemba 2016.

Aidha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya alisema TRA imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma zake na kuwafikia walipakodi kwa ukaribu zaidi ili kuondoa usumbufu na kuokoa muda wa upatikanaji wa huduma hizo.

“TRA kwa kuhakikisha walipakodi wanapata huduma iliyo bora imeanzisha vituo vingi vya kodi katika jiji la Dar es Salaam na nchi nzima ili  walipakodi wapate  huduma stahiki na ya haki na kuiwezesha Serikali kupata mapato yake kwa mendeleo ya Taifa letu” Alisema, Mwandubya.

Posted by MROKI On Wednesday, October 26, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo