Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2016

Mkuu wa wilaya kakokonko Kanali Hosea Ndagala akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya NMB na kukabidhiwa na Meneja wa NMB Kakonko Leonard Ngaya. wanaoshuihudia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kankonko, Dk Tuluba (kulia) na  Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo, Mwakabibi Lusubilo.
Mkuu wa wilaya kakokonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya NMB. Wengine pichani ni kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kankonko, Dk Tuluba, Meneja wa NMB Kakonko Leonard Ngaya, Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo, Mwakabibi Lusubilo na Ofisa huduma kwa Wateja wa NMB, Malima Mumanga.
Meneja wa NMB Kakonko Leonard Ngaya akizungumza. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, kanali Hosea Ndagala na kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya.
******************
BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vitanda na magodoro kwa ajili ya wodi ya wazazi vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni Tano katika kituo cha Afya Mganza Wilayani Kakonko mkoani Kigoma ambacho kinatumika kama hospitali ya Wilaya.

Msaada huo umekabidhiwa leo na Meneja wa NMB tawi la kakonko, Leonard Ngaya kwa niaba ya Meneja NMB Kanda ya Magharibi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo la kituo cha Afya cha Mganza Kakonko.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Ngaya alisema benki ya NMB imetoa msaada huo kufuatia maombi yaliyotolewa na Halmashuri hiyo kutokana na   upungufu wa vitanda na magodoro katika kituo hicho cha afya.

Kwa mujibu ya maelezo ya Ngaya benki hiyo imekuwa ikisaidia msaada miradi mbalimbali ya maendeleo  kwenye jamii katika sekta ya Elimu,afya na majanga yanapojitokeza ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida wanayopata Kwa jamii  ambayo ndiyo wateja wa sekta hiyo.

Aidha hii ni mara ya pili kwa benki hiyo kutoa msaada wa aina hiyo na aliahidi kuwa NMB itaendelea kutoa msaada zaidi katika wilaya hiyo pale itakapoombwa kufanya hivyo.

Mkuu wa wilaya wa Kakonko Kanali Hosea Ndagala mara baada ya kuupokea msaada huo alisema kuwa msaada huo umekuja katika wakati muafaka kwa kuwa utasaidia kuondoa tatizo la upungufu wa vitanda na magodoro uliyopo katika kituo hicho cha afya.

Kanali Ndagala ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vifaa hivyo na vingine vinatunzwa ili viendelee kutoa huduma na kusaidia wananchi wa Kakonko na mewataka kuboresha huduma ili kupunguza vifo vya akinamama na mtoto.

 Ndagala ametoa rai kwa wadau wengine kuiga mfano wa benki hiyo ya kuchangia katika shughuli za kijamii zinazoikabili wilaya hiyo.

Mganga mKuu wa kituo hicho  Muganza alisema msaada huu wa benki ya nmb utasaidia kupunguza zaidi vifo vya akinamama wajawazito kujifungulia katika mazingira mazuri na kuondoa tattizo la wagonjwa kulala wawili wawili.
Posted by MROKI On Wednesday, October 26, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo