Nafasi Ya Matangazo

October 25, 2016



Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) 
Beng’i Issa
******
 Na Ally Daud-MAELEZO.
WATANZANIA zaidi ya asilimia 70 wamepewa kipaumbele  kushiriki katika shughuli za kujenga uchumi wa nchi kufikia uchumi wa kati katika kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi mpaka kufikia mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng’i Issa wakati wa ufunguzi wa ripoti ya Tathimini  ya Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tunataka kufikia 2020 watanzania asilimia zaidi ya 70 waweze kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kufikia katika uchumi wa kati ili kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini” amesema  Issa.

Aidha Issa amesema kuwa watanzania wanatakiwa washiriki katika shughuli za kiuchumi na wasitegemee zaidi wawekezaji kutoka nje ili kuifanya Tanzania iendelee kiuchumi kutoka ngazi ya mmojammoja  hadi kufikia maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Meneja wa Utafiti na ufatiliaji wa Sera hiyo kutoka NEEC, Frola Kajela amesema kuwa Serikali imeandaa sera hiyo ili kuwezesha watanzania kutumia rasilimiali zilizopo katika kuinua uchumi wa nchi na kuweza kumilikiwa na watanzania wenyewe.

“Sera hii inalenga zaidi kwa watanzania kumiliki uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini ili kujishughulisha katika kuleta maendeleo ya nchi kwa jamii na taifa kwa ujumla mpaka kufikia 2020” alisema  Kajela.

Aidha Bi. Kajela amesema kuwa sera hiyo inafanyiwa maboresho ili kuweza kuwafikia watanzania wote katika kuelewa na kumiliki uchumi kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza  mpango wa serikali uliyowekwa kuhakikisha watanzania wanajiinua kiuchumi.
Posted by MROKI On Tuesday, October 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo