Nafasi Ya Matangazo

August 31, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)  Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua   litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi . 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya . 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio  la kupatwa  kwa jua linalotarajia kuonekana Septemba mosi  mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha 

Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa


Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete  anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni  fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa  eneo la Ihefu   linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo   ina vivutio vingi, hivyo amewataka  wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .


Posted by MROKI On Wednesday, August 31, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo