Nafasi Ya Matangazo

August 25, 2016

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba jana aliongoza, viongozi wa Serikali, Makamishna wa Polisi na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam katika kuaga miili ya Askari Polisi watatu kati ya wanne waliouwawa juzi katika shambulio la ujambazi.

Askari wa nne wa Jeshi la Polisi waliuwawa jumanne usiku katika eneo la Benki ya CRDB, Mbande, Kata ya Chamanzi, Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam ambapo watu wenye silaha waliwavamia wakiwa kazini na kuwauwa na kupora bunduki mbili aina ya SMG na risasi 60.

Miili ya Askari walioagwa jana katika viwanja vya Polisi Barabara ya Kilwa ni pamoja na Koplo Yahaya Malima aliyesafirishwa kwenda kuzikwa kijiji cha Kibuta, Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Tito Mapunda aliyesafirishwa kwenda Kijiji cha Migoli, Wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na Gaston Lupanga aliyesafirishwa kwenda mjini Songea mkoani Ruvuma kwa maziko. 

Askari mwingine Koplo Khatib Ame Pandu alisafirishwa Jumatano jioni kwenda Zanzibar ambapo maziko yalifanyika siku hiyohiyo usiku.
Askari wakiwa wamebeba moja ya sanduku lililohifadhi mwili wa Askari
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa kuaga miili hiyo ya Askari.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IJP) Ernest Mangu akizungumza
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akitoa heshima za mwisho kwa miili ya askari walio uwawa katika shambulizi dhidi ya Polisi huko Mbande.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akiwafariji wafiwa.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akiwafariji wafiwa.
Askari wakimsaidia mmoja wa wafiwa.
Posted by MROKI On Thursday, August 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo