Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2016

KAMPENI ya mawakala wa kuuza vinywaji vya Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayojulikana kama “Nunua, Uza, Shinda na Konyagi ambayo itawezesha washindi kujipatia malori ya usambazaji bidhaa inazidi kupamba moto.

Baadhi ya  mawakala wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali  wanaendelea na mikakati mizito ya usambazaji vinywaji ili kufikia lengo la kuingia kwenye droo kila mmoja akiwa amepania kujishindia lori la zawadi ya kampeni hii.

Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe, amesema kuwa baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi kila kanda ambao umekuwa na mafanikio na kuwashirikisha mawakala wanaouza bidhaa za kampuni hivi sasa kazi kubwa imebaki kwao kufanya mauzo na kufikia viwango vya kuingia kwenye droo ya kupata washindi.

“Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kubuni kampeni hii ni  kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wawili katika kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji aina ya Eicher  yenye uzito wa tani 3 pia tunazo zawadi mbalimbali ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuongeza motisha kwao katika kipindi hiki cha kampeni”alisema.

Alisema kampeni itadumu kwa kipindi cha wiki 12 na wasambazaji wanaoshiriki wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu . “Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.

Baadhi ya mawakala wamepongeza jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa za promosheni ambazo zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya zawadi ndogondogo  zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.

Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya Konyagi kanda ya Ziwa aliyejitambulisha kama John Masanja amesema kuwa japo sio mawakala wote watapata malori lakini watakaobahatika kushinda watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha biashara kukua. 

“Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo vya kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema.

Posted by MROKI On Wednesday, August 03, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo